Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Shule ya Msingi Engira iliyopo kata ya Themi jijini Arusha inakabiliwa na tatizo la
ukosefu wa maji ya kutosha licha ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi zaidi ya
600 hali inayoweza kukwamisha shughuli za usafi wa mazingira na afya za
wanafunzi.
Mkuu wa Shule hiyo Saimon Siara amesema kuwa shule hiyo ina
uhitaji mkubwa wa maji kwa ajili ya
matumizi mbali mbali na kwamba tatizo
hilo lisipotatuliwa huenda wanafunzi wakapata madhara ya kiafya.
“Tunahitaji maji kwa ajili ya kupikia,kunywa ,kuweka kwenye
vyoo vya shule ili kuboresha usafi hasa watoto wanapokuwa mashuleni” Alisema
Mkuu wa Shule
Ameeleza kuwa changamoto zinaikabili shule hiyo ni ukosefu
wa sehemu ya kula hususani bwalo hivyo watoto hutumia madarasa na hata
mazingira ya nje ambayo si salama .
Katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo Kampuni ya Bia ya
TBL imetoa kiasi cha shilingi milioni 9.8 ili kusaidia ujenzi wa kisima hicho
muhimu ikiwa ni moja kati ya shughuli zake za kuisaidia jamii
inayowazunguka,fedha zilizotolewa na Mkuu wa kiwanda cha bia TBL kanda ya
Kaskazini Salvatory Rweyemamu na
kukabidhiwa kwa Diwani wa Kata ya Themi Wallance Kinabo.
Diwani wa Kinabo amesema kuwa kampuni hiyo imekua mfano
katika kuchangia maendeleo ya jamii na kuwataka waendelee kuwa wadau muhimu wa
maendeleo ya jamii.
“Kwa muda mrefu shule hii imekosa kisima cha maji lakini
sasa tumaini lipo tunaamini baada ya wiki mbili ujenzi wa kisima utaanza na
wanafunzi watapata huduma hiyo muhimu” Alisema Kinabo
Diwani wa kata ya Themi Wallance Kinabo akipokea cheki ya shilingi
milioni 9.8 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kisima cha Maji katika shule
ya msingi Engira kutoka kwa Mkuu wa kiwanda cha bia TBL kanda ya
Kaskazini Salvatory Rweyemamu,katikati ni Mkuu wa shule hiyo Saimon
Siara .Picha na Ferdinand Shayo
Post a Comment