PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SERIKALI YA CHINA YAKANUSHA KUHUSIKA NA UJANGILI WA PEMBE ZA NDOVU ZA TANZANIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Waziri wa Mali asili na Utali,Lazaro Nyalandu akizungumza  Waziri wa Mali asili na Utali,Lazaro Nyaland...


 
Waziri wa Mali asili na Utali,Lazaro Nyalandu akizungumza 


Waziri wa Mali asili na Utali,Lazaro Nyalandu akizungumza 



Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Mali asili,Ardhi na Mazingira,James Lembeli

Wajumbe wa Mkutano



Balozi wa China nchini Tanzania,Lu Youqing

Serikali ya China imelaani vikali uzushi uliotolewa na vyombo vya habari vya magharibi kutuhumu ndege ya Rais wao  kutumika kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.

Akizungumza leo mjini Arusha Balozi wa China, Lu Youqing amesema kuwa huo ni uongo mkubwa ambao ulikuwa na nia ya kutia aibu taifa lake na Tanzania kwa ujumla.

Alisema kwamba China hutoa adhabu kali kwa mtu anayefanya uovu kama ujangili, "Kama mwandishi angeweza kuthibitisha hao maafisa wangechukuliwa hatua kali, na hilo liko ndani ya uwezo wangu kwanini ameshindwa kuwataja?"

Lu amesema kwamba udhabu kama hiyo si kwa mtu aliyekutwa na nyara tu bali hata kwa muongo, mwandishi huyo ni muongo na anatakiwa aadhibiwe.

Waziri wa maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu aliunga mkono kauli hiyo na kusema kuwa ilikuwa na nia ya kuchafua hali ya hewa kutokana na mkutano wa kimataifa ulioanza leo jijini Arusha.

"Hata tulipokwenda na Rais Jakaya Kikwete jijini London kwa mkutano wa kimataifa juu ya ujangili gazeti la Dail Mail lilita habari za kashfa kuhusu Tanzania siku moja kabla ya mkutano na hii leo ndio limetokea,"alisema Nyalandu

Aliwashukuru  wadau wa uhifadhi ambao kwa kiwango kikubwa wamehudhuria kikao hicho  muhimu  ambacho kitaleta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya ujangili.

Kikao hicho kilihudhuriwa na mawaziri kutoka nchi tisa za Afrika ukanda wa bahari ya Hindi na Afrika Mashariki na Kati pamoja na wawakilishi wa mashirika mbalimbali na balozi wa nchi nyingi wanaowakilisha nchi zao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top