PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MWANAMUZIKI NGULI WA TWANGA PEPETA; AMIGOLAS KUZIKWA LEO MAKABURI YA KISUTU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Mwimbaji wa zamani wa bendi ya African Stars, Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jan...



 


Mwimbaji wa zamani wa bendi ya African Stars, Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo, anatarajia kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.


Amigolas alilazwa Hospitali ya Muhimbili siku nne zilizopita kwa matatizo ya moyo ambapo taratibu za kufanyiwa upasuaji zilikuwa zikiandaliwa na kukutwa na umauti kabla ya kufanyiwa upasuaji.


Hadi umauti unamkuta Amigolas, alikuwa ni mwimbaji wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


Amigolas alikuwa mmoja wa wanamuziki waasisi wa Twanga Pepeta, akaitumikia kwa uaminifu mkubwa kwa miaka mingi kabla ya mwanzoni mwa mwaka huu yeye na wenzake kadhaa kuanzisha Super Stars Band ambayo baadae ikachukuliwa na JKT na kuwa Ruvu Stars Band.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top