PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MADEREVA WALALAMIKIA MSONGAMANO WA MAGARI KISIWANI PEMBA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
   MADEREVA wa magari ya kubeba abiria Kisiwani Pemba, wameitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kulitafutia ufumbuzi tatizo la msongam...
  


MADEREVA wa magari ya kubeba abiria Kisiwani Pemba, wameitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kulitafutia ufumbuzi tatizo la msongamano wa magari katikati ya mji ambalo limeelezwa kuwa limekuwa likiongezeka kila siku.

Wakizungumza na FikraPevu Octoba 16,2014 madereva hao wameeleza kwamba hali hiyo imekuwa ikijitokeza hususani katika Kituo cha Mji wa Chakechake Pemba, na kwamba hali hiyo imekuwa ikileta adha kwa watumiaji wake mara kwa mara.

“Hili tatizo linametusumbua kwa muda mrefu na sio kwamba limeanza leo tumewashirikisha hata Masheha ili waihamasishe serikali pamoja na Madiwani lakini bado hatujaona juhudi zao ndio maana tunazidi kupaza sauti ili tuondokane na masuala haya” alikaririwa na FikraPevu mmoja wa madereva hao.

FikraPevu imezungumza na abiria wanaotumia kituo hicho na kueleza kwamba msongamano huo unasababisha kero kwa watumiaji wa kituo hicho na kwamba wakati mwingine wanapokutana na kadhia hiyo wanajibadilisha kuwa Askari wa Usalama Barabarani kwa ajili ya kujua njia gani wanayopaswa kuitumia.

Katibu wa Jumuiya ya madereva wa Kusini Pemba, Hafidh Salim, amesema kwamba bila kuwepo kwa kituo kipya, msongamano huo utaendelea kutokana na maendeleo yanayokuwa kwa kasi katika mji huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Haruna Ibrahim Said, amekiri kuwepo na tatizo hilo ambapo amebainisha kwamba tayari serikali imepata eneo la kujenga kituo kipya cha magari hayo,huku akiwaomba wananchi mjini humo kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kufuatilia mchakato huo.
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top