PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HABARI PICHA-NAIBU WAZIRI WA KILIMO GODIFREY ZAMBI AKIWEKA GUNIA KWENYE MASHINE YA KUSAFISHA MBEGU jijini arusha
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Godifrey Zambi  Akiongozana na Viongozi wa kampuni ya  mbegu ya Seedco ,kushoto ni Meneja Masoko wa Ka...
Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Godifrey Zambi  Akiongozana na Viongozi wa kampuni ya  mbegu ya Seedco ,kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Seedco Frank Wenga ,wakwanza kulia ni Afisa Mauzo Mwandamizi wa kampuni hiyo mkoa wa Manyara Kasim Nyaki na Mwenyekiti wa Seed Co-Afrika Mashariki- Bw. Mike Ndorro wapili kulia .Katika uzinduzi wa kiwanda chao kipya uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha .Picha na Ferdinand Shayo

Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Godifrey Zambi akiweka gunia kwenye mashine ya kusafisha mbegu katika uzinduzi wa kiwanda kipya cha kuzalisha mbegu kilichopo kata ya Kisongo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha ,wakwanza mstari wa mbele ni Afisa Mauzo Mwandamizi wa kampuni hiyo mkoa wa Manyara Kasim Nyaki.Ferdinand Shayo

Kampuni ya mbegu ya Seedco imezindua kiwanda kipya cha kuzalisha mbegu bora za mahindi na nafaka nyingine kitakachowasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija na kupata mazao mengi.

Uzinduzi huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Godifrey Zambi ambaye alifungua rasmi kiwanda hicho ,Amesema kuwa tasnia ya mbegu ni tasnia muhimu katika ukuaji wa sekta ya kilimo hiyo amewataka wazalishaji mbegu kuongeza tija ili kukuza kilimo.


Ameeleza kuwa kampuni hiyo imetimiza matakwa ya serikali kwa kwa kuandaa na kuzalisha mbegu nchini badala ya kuagiza kutoka nje na kuzilipia kwa fedha za kigeni .


"Mbegu hizi zinazoandaliwa na kuzalishwa ndani ya nchi zinasambazwa kwa bei rahisi na wakulima wanazipata kwa bei rahisi tofauti na zile zinazoagizwa kutoka nje bei yake huwa juu" Alisema Waziri huyo


Mwakilishi wa Bodi ya Seedco,Profesa Kalunde Simbuge amesema kuwa mbegu hizo bora zinazozalishwa na kiwanda hicho zitawasaidia wakulima kuzalisha chakula cha kutosha na ziada kwa ajili ya kuuza na kujipatia kipato.


Profesa Kalunde anafafanua kuwa wakulima wana jukumu kubwa la kuilisha jamii hivyo wanahitaji  mbegu bora zinazoendana na mazingira yao.


Mkulima kutoka Wilaya ya Hai Joel Nkya amesema kuwa ufunguzi wa kiwanda hicho utakidhi mahitaji ya mbegu bora hasa kwa wakulima walioko vijijini.Amewashauri wakulima wenzake kuacha kuona kuwa mbegu halisi ni ghali na kuingia kwenye mtego wa kuuziwa mbegu feki kwa bei rahisi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top