Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishiriki katika ujenzi wa banda la kisasa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku katika kituo
cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Bunju, jijini Dar es
salaam.Wafanyaka hao walishiriki katika ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.
Katibu
wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa cha Bunju jijini Dar
es Salaam, Bw.Omar Abdul Kyaruzi(kushoto)akimpa maezo Meneja wa
Vodacom Foundation,Grace Lyon jinsi ujenzi wa banda la kisasa kwa ajili
ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku unaufadhiliwa na taasisi ya
Vodacom foundation unavyoendelea kituoni hapo walipotembelewa na
wafanyakazi wa Vodacom katika kushiriki kwenye ujenzi huo ikiwa ni
sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.
Wafanyakazi wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,wakishiriki katika ujenzi wa banda la kisasa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku kwenye kituo
cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Bunju, jijini Dar es
salaam,Wafanyakazi hao walishiriki katika ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.
Vodacom yaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kufadhili mradi
wa ufugaji kuku
“Mhisani anayekusaidia kujijengea uwezo wa kujitegemea ni muhimu sana
kuliko Yule anayekupatia msaada kila siku bila kukujengea uwezo wa
kusimama mwenyewe na kujitegemea”anasema Bw.Omar Abdul Kyaruzi Katibu wa
kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo eneo la Boko
wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam kutokana na kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania kusaidia kituo hicho kujenga banda la kisasa
kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku.
Mbali na kufadhili ujenzi wa banda la kuku pia wafanyakazi wa
Vodacom Tanzania katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea
wamejitolea muda wao kushiriki katika ujenzi wa banda hilo la kisasa
ambalo lina ukubwa wa kufugiwa kuku wapatao 2,000 kwa pamoja.
Afisa Mwandamizi wa Vodacom Tanzania kutoka kitengo cha
Huduma kwa wateja Benson Megehema, amesema kuwa wiki hii mbalimbali na kuongea
na wateja na kuwaelimisha huduma bora zinazotolewa na kampuni pia wameona ni
muhimu kutenga muda wao kusaidia shughuli za kijamii hususani kusaidia wahitaji
kwenye jamii.
“Kwetu Vodacom kusaidia jamii ni moja ya sera yetu na siku zote
tutakuwa mstari wa mbele kusaidia jamii tunayoishi na kufanyia biashara na
tunaamini kuwa kusaidia sio kutoa fedha tu bali ni kujitoa muda wetu pia kujumwika
na watoto hawa wapatao themanini na kitu na kuweza kusaidia shughuli za kijamii
kwanAi tunatambua uhitaji wetu ni muhimu sana kwa watoto hawa tukiwa na lengo la mradi huu
kuweza kuwasaidia katika mahitaji yao ya hapa na pale”Anasema Magehema.
Kwa upande wake Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha
Mwandaliwa,Bw.Omar Kyaruzi,alisema kuwa wanashukuru kampuni ya Vodacom Tanzania
kwa kuona umuhimu wa kuweajengea banda kwa ajili ya uanzishaji wa mradi
wa ufugaji wa kuku.
Pia aliongeza kuwa wamefarijika kuona wafanyakazi wa Vodacom
wanaacha kazi zao ofisini na kuungana na mafundi katika kazi ya ujenzi
“Suala hili limetutia moyo sana hata watoto tunaowalea wamejifunza kuwa msaada
sio kutoa fedha peke yake bali kutumia muda wako kusaidia jamii ni msaada
mkubwa kwa kuwa wakati ni pesa”Alisema Kyaruzi.
Kyaruzi alisema kuwa Kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa
kinatoa malezi kwa watoto yatima na kimekuwa kikitegemea kujendesha kupitia
misaada mbalimbali inayotolewa na wafadhili.
Post a Comment