Siku moja baada ya viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutangaza mpango wa kusaini makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, imeelezwa kuwa endapo utachukua dola, utarejea upya mchakato wa kuandika Katiba.
Hayo yalisemwa kwa nyakati tofauti na viongozi wa
mabaraza ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza juzi.
Walisema mchakato huo utarudiwa kwa kutumia Rasimu
ya Katiba iliyoandaliwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya
Katibailiyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Pia, viongozi hao waliwataka Watanzania waliofikisha umri wa kupiga kura, kujiandikisha katika Daftari la Wapigakura mara baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuanza uandikishaji huo.
Pia, viongozi hao waliwataka Watanzania waliofikisha umri wa kupiga kura, kujiandikisha katika Daftari la Wapigakura mara baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuanza uandikishaji huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema
(Bawacha), Halima Mdee akihutubia mamia ya wananchi waliofurika kwenye
viwanja hivyo, alisema maoni ya wananchi waliyoyatoa mbele ya Tume ya
Warioba yamewekwa kando kwa masilahi ya wachache.
“Ni kwamba, Ukawa tukishinda uchaguzi ujao
mwakani, mwaka 2016, mchakato wa Katiba utaanza upya kwa kutumia Rasimu
ya Jaji Warioba... Warioba na wenzake walitengeneza Rasimu yenye manufaa
kwa Taifa zima si genge la watu wachache,” alisema Mdee.
“Sasa (mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew)
Chenge na wenzake kwa kuona itawabana katika maeneo ya uwazi na maadili
wameichakachua.
“Hatuwezi kukubali kuiona asilimia 80 ya maoni
yenu mliyoyatoa kwa Jaji Warioba ikiwekwa kando na kuingizwa yao...
ikija ikataeni, ikataeni, tupeni kule.
Kama theluthi mbili wamechakachua
katika kura ya maoni, watakiona,” alisisitiza.
Nae Katibu mwenezi wa Bavicha, Edward Simbeye alisema
wanachokitaka katika Katiba Inayopendekezwa ni huduma bora za afya na si
mabomu ya machozi, maji safi na chaki shuleni si virungu vya polisi.
“Polisi wanatumika vibaya. Ili kuhakikisha
tunajikomboa kutoka utumwa wa Serikali ya CCM, tujitokeze kujiandikisha
katika Daftari la Wapigakura ili tuanze kuiondoa CCM kuanzia uchaguzi wa
Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, ndiyo tuseme
kwaheri CCM,” alisema Simbeye.
Naibu katibu mkuu wa Bawacha (Bara), Kunti Yusuph
alisema Katiba Inayopendekezwa iliyokabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete,
imeshindwa kuziba mianya ya rushwa na maadili kwa viongozi wa umma na
badala yake kujiwekea mazingira ya kuendelea kuwanyonya Watanzania.
“Tukicheza na Katiba hii waliyoipendekeza ma-CCM,
ikipita tutakuwa tumejichimbia kaburi wenyewe... hatutaki na tutaipinga
kona zote. Tumeanza hapa tutazunguka nchi nzima,” alisema Yusuph.
Mbunge wa viti maalumu (CUF), Mkiwa Kimwanga
alisema kazi inayofanywa na Ukawa itaendelea kuanzia chaguzi za Serikali
za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ili kuhakikisha CCM haiendelei kuwanyanyasa
wananchi.
“Katika sherehe za Uhuru wa Tanganyika mwaka huu, vijana wa halaiki walitumia Sh775 milioni, weka mbali polisi, ndege za kivita na mengineyo, halafu leo mnaambiwa mchangie ujenzi wa maabara, hamuoni kama huu ni wizi,” alihoji Mkiwa.
“Katika sherehe za Uhuru wa Tanganyika mwaka huu, vijana wa halaiki walitumia Sh775 milioni, weka mbali polisi, ndege za kivita na mengineyo, halafu leo mnaambiwa mchangie ujenzi wa maabara, hamuoni kama huu ni wizi,” alihoji Mkiwa.
Post a Comment