Mkuu
wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji
(UNCDF), Peter Malika akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa
miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha
(LFI) unaosimamiwa na mfuko huo katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu
MATAIFA manane yaliyopo katika nchi zinazoendelea zitaanikizwa mafanikio ya Tanzania katika utekelezaji wa programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) inayosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF).
Pamoja
na upelekaji wa maarifa yaliyopatikana nchini Tanzania katika
utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi huo ambao ulianza mwaka 2012 na
kumalizikia 2015, Watanzania ndio watakaotumika kupeleka maarifa mapya.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa UNCDF, Peter Malika
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu warsha ya siku tatu
inayofanywa na UNCDF iliyolenga kuwaelimisha wadau mbalimbali
wanaohusika na programu hiyo.
Wadau hao ni waandaaji wa miradi, watoa fedha na wasimamizi wanaofanya maamuzi.
Alisema
baada ya mafanikio ya mradi huo, UNCDF imemua Tanzania kuwa makao makuu
ya LFI na kwamba watanzania baada ya kuonesha uwezo wa dhana za LFI,
mafanikio hayo katika mataifa mengine.
Mataifa
yaliyoelezwa kupelekewa utaalamu wa watanzania kuanzia awamu ya pili
inayotarajiwa kuanza mwakani hadi mwaka 2017 ni Uganda, Benin, Senegal
na Bangladesh.
Majadiliano ya nchi nyingine tatu bado yanaendelea na zitapatikana baada ya serikali hizo kukubali kuwepo kwa mradi huo, alisema Malika.
Alisisitiza kwamba program ya LFI inatekelezwa kwa kushirikiana na serikali na hapa Tanzania inafanyika kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI).
Katika
utekelezaji wa program hiyo LFI imesaidia miradi kadhaa yenye
kipaumbele inayogusa miundombinu ya nishati, kilimo na mawasiliano.
Kwa mujibu wa Malika kuna miradi 25 yenye maslahi kwa umma ambayo imewezeshwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Akifafanua
zaidi alisema miradi hiyo 25 ya miundombinu iliyoanzishwa na wawekezaji
wa umma na binafsi iko katika hatua mbalimbali za uendelezaji.
Aidha alisema miradi hiyo imetawanyika katika
sekta mbalimbali zikiwemo za usindikaji bidhaa za kilimo, nishati,
miundo mbinu ya utoaji huduma za jamii, mawasiliano na uzalishaji
viwandani katika mikoa 10 kote nchini.
Mtaalamu
wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja
wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner akitoa mada yenye
kuainisha zana za ubunifu zikiwemo masuluhisho wakati wa uhaba wa fedha,
mkakati ya kukabili athari, mtiririko wa uandaaji mikataba na masharti
na kanuni za msingi zinazoweza kujitokeza katika kila mkataba kwenye
warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandazi wa miradi chini ya programu ya
Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na mfuko huo
katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.
Hadi
kufikia Septemba mwaka huu miradi mitano iliyopiga hatua kubwa zaidi
ilitarajiwa kufikia kikomo cha bajeti yake katika miezi sita hadi tisa
ijayo ambapo dola milioni 26 za mtaji wa ndani katika muundo wa mkopo na
misaada ipatayo dola milioni 3 ilihamasishwa.
Msaada
wa LFI kwa miradi iko katika muundo wa utaalamu wa kiufundi, kutoa
amana, misaada ya kifedha na aina nyingine ya mikopo ambayo inahitajika
sana kwa miradi midogo na ya kati ya miundombinu ili ivutie uwekezaji.
LFI
imeundwa kuhamasisha ukuaji endelevu, jumuishi na wenye usawa kwa
kufungua fursa za uwekezaji ili kuleta mabadiliko chanya na kusaidia
miradi kupata fedha kupitia sekta binafsi na hasa masoko ya mitaji.
UNCDF
yenye jukumu la pekee kuhusiana na fedha katika mfumo wa Umoja wa
Mataifa, shirika hili limelenga kutoa msaada wa mtaji wa kuwekeza na wa
kiufundi katika seklta ya umma na binafsi.
Aidha
imepewa uwezo wa kutoa fedha za uwekezaji katika muundo wa misaada,
mikopo na uwezeshaji wa ukopaji na utaalamu wa kiufundi katika kuandaa
taarifa ya mradi kuhusu uendelevu na kujenga uwezo wa kuondoa hatari ya
kuporomoka.
Kazi
ya UNCDF ni kuhakikisha pia watu katika mikoa na maeneo yote
wananufaika na ukuaji wa uchumi kwa kushughulikia changamoto zao hasa
maeneo ya pembezoni mwa mji na vijiji.
Na
katika hilo Malika alisema lengo kuu ni kuhakikisha kwamba miundombinu
hasa ya maeneo ya vijijini ambayo haiwezi kupata kirahisi ridhaa ya
taasisi za kifedha au utekelezaji wa serikali kuu inawezeshwa kwa
kuitafutia andiko madhubiti na kuelekeza namna ya kupata fedha za
utekelezaji.
“Kwa
maneno mengine, miradi ile ambayo pengine isingekopesheka athari zake
zinapunguzwa na kuingizwa katika hatua ya kuwa tayari kupokea uwekezaji
ambapo inaadaliwa ili ipate mtaji wa kibiashara” alisema Malika.
Mkurugenzi
wa Nelwa's Gelato wauzaji wa watengenezaji wa Ice Cream, Bi. Mercy
Kitomari akiuliza swali muwasilishaji mada Mtaalamu wa nishati mbadala
na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji
Mitaji (UNCDF), Michael Feldner wakati wa warsha hiyo.
Matokeo
ya jumla ya LFI, kwa mujibu wa Malika ni kuongezeka kwa ufanisi wa
rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya hapa nchini
kupitia uhamasishaji kwanza kabisa wa mtaji binafsi kutoka nchini na
masoko ya mitaji ili kuwezesha na kuhamasisha maendeleo ya mahalia
yaliyo jumuishi na endelevu.
Akizungumzia
warsha hiyo ya siku tatu ambayo imeanza leo, Malika alisema kwamba
zaidi ya watu 120 watashiriki wakiwamo waandaaji miradi na taasisi za
kifedha.
Mafunzo
ya leo ambayo yalihusu waandaaji miradi waliwezeshwa na mtaalamu
nishati mbadala Michael Feldner ambaye pia ni mshauri wa masuala ya
kifedha wa UNCDF.
Mtoa
mada huyo aliainisha zana za ubunifu zikiwemo masuluhisho wakati wa
uhaba wa fedha , mkakati ya kukabili athari, mtiririko wa uandaaji
mikataba na masharti na kanuni za msingi zinazoweza kujitokeza katika
kila mkataba.
Mafunzo
mengine yatagusa watu wa fedha wanaopokea maandiko na kuyafanyia
tathmini, ambayo yatafanyika kesho na kuishia na watoa maamuzi katika
taasisi hizo kuhusu mikopo iliyoombwa.
Mtaalamu
wa masuala ya fedha wa programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji
Fedha (LFI) Abraham Byamungu akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa warsha ya
siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada
za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa
mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) katika hoteli ya Serena mjini Dar es
Salaam leo.
Kutoka
kushoto ni Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa
Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika, Bw. Imanuel Muro wa UNCDF
pamoja na Ofisa Msaidizi anayeshughulikia masuala ya fedha Program ya
LFI kutoka UNCDF, Bw. Oscar Kanyenye wakifuatilia mada zilizokuwa
zikiwasilishwa na Mtaalamu wa nishati mbadala na mshauri wa masuala
ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF),
Michael Feldner (hayupo pichani).
Sehemu
ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha
ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada
za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na mfuko huo katika
hoteli ya Serena mjini Dar es salaam leo.
Washiriki
wa warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu
ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na Mfuko wa
Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) wakisikiliza mada katika
hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.
Mshiriki
kutoka Ileje Mbeya, Bw. Joseph Mchome akitoa maoni yake kwenye warsha
ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada
za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa
mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) katika hoteli ya Serena mjini Dar es
Salaam leo.
Mkuu
wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji
(UNCDF), Peter Malika akizungumza na waandishi wa habari kuhusu warsha
ya siku tatu inayofanywa na UNCDF iliyolenga kuwaelimisha wadau
mbalimbali wanaohusika na programu hiyo.
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akibadilishana mawazo na Mtaalamu
wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja
wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner kwenye warsha
hiyo.
Post a Comment