PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Serikali hutumia bilioni 40 kila mwezi kulipia pango za majengo inayoyatumia Dar
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
TAKRIBANI bilioni 40 hutumiwa na serikali kila mwezi kwa ajili ya kulipia pango za majengo yanayotumiwa na Wizara, Taasisi na Idara ...





TAKRIBANI bilioni 40 hutumiwa na serikali kila mwezi kwa ajili ya kulipia pango za majengo yanayotumiwa na Wizara, Taasisi na Idara za umma zikiwemo nyumba wanazoishi viongozi wakuu serikalini katika mkoa wa Dar es Salaam pekee.

Taarifa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya habari zinaeleza kuwa wakati wananchi wanakabiliwa na matatizo lukuki katika maeneo wanayoishi, fedha hizo hutumika kwa ajili ya kulipia sehemu hizo hali inayotajwa kuwa ni ufujaji wa fedha za umma ililinganishwa na maeneo yanayokabiliwa na matatizo kadha wa kadha ikiwemo wanafunzi kujisomea katika mazingira magumu bila kutafutiwa ufumbuzi.

Habari za ndani zilizoifikia zinaeleza kwamba Ofisi ya Idara ya Ushauri kutoka Ofisi ya Wakala wa Majengo Tanzania, inalenga kujenga nyumba za watumishi pekee ili kuinasua serikali katika wimbi hilo na kwa kuanza wakala huyo ameweka mikakati ya kukabiliana na hali hiyo katika kipindi cha miaka minne (4) ijayo.

“Kwa sasa wakala anategemea kuanzisha mradi wa kujenga nyumba kwa ajili ya watumishi wa serikali na nyumba hizi zitauzwa kwa bei nafuu kwa hawa watumishi (haijawekwa wazi mradi utaanza lini) na ieleweke tofauti kati ya kikosi hiki na taasisi au mifuko mingine ya umma inayojenga nyumba za gharama nafuu ni kuwa wakala wa Majengo Tanzania, umelenga kuwajengea watumishi wa umma pekee ili hizi gharama za pango ziondolewe kwa asilimia fulani” kilieleza chanzo chetu.

Habari kutoka serikalini zinaeleza kwamba wakala huyo anakusudia kujenga nyumba 10,000 sawa na nyumba 2,500 kila mwaka katika kipindi cha miaka minne kuanzia sasa, ambapo kada ya walimu itapewa kutokana na kuwa moja ya kada inayokabiliwa na ukosefu wa nyumba za watumishi.

Kwa mujibu wa habari hizo, serikali imekuwa ikitumia zaidi ya kiwango hicho cha fedha wakati matatizo mengi yakiwa yanawakabili wananchi kutokana na kilio cha muda mrefu kilichopo katika sekta tofauti, ikiwemo miundombinu ya barabara, elimu, afya na hali duni ya maisha ya baadhi ya wakazi wengi nchini.

Wakazi wa jiji hilo akiwemo, Ramadhani Josephati, wameonyesha wasiwasi juu ya kiwango hicho kuwa kinaingia kwenye mifuko ya watumishi wasio waaminifu, huku wakitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Prevention and Combating of Corruption Bureau (TAKUKURU)na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutolifumbia macho suala hilo kwani ni ubadhilifu wa fedha za umma na kwamba sio mara ya kwanza sakata hili kujitokeza.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top