Waziri
mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akihutubia semina
ya ardhi wilayani Monduli jana katika hoteli ya Emanyata ambapo alisema
kuuza ardhi ni sawa na kuuza utajiri na kununua umasikini.Wilaya ya
Monduli ni moja kati ya wilaya zenye matatizo makubwa ya ardhi.
Lowassa aliwaonya viongozi wa vijiji, ccm na wakuu wa kimila kuacha tabia ya kuuza ardhi hususan za wajane.
Waziri
Mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa amewanyooshea
vidole viongozi wa kimila(malaigwanani),viongozi wa vijiji na wale wa
ccm wilayani humo, kuwa wanalaumiwa kwa kushiriki katika uuzaji ardhi
kinyume na sheria.
Akifungua
semina ya siku mbili juu ya ardhi kwenye ukumbi wa hoteli ya Emanyata
mjini Monduli,Mh Lowassa amesema shutuma hizo zimekuwa nyingi kwa kuuza
utajiri(ardhi) na kununua umasikini.
"Walikuja
pale nyumbani kwangu wale watu wa maombezi(walokole), moja ya mambo
waliyoyalalamikia ni uzwaji wa ardhi.wakaniambia hivi Mh mbunge hamuoni
viongozi, vijiji an ccm pamoja na malaigwanan wanavyopokea rushwa na
kuuza ardhi? Wanavyowadhulumu wajane?" Alisema Lowassa na kuongeza
akaona kuna umuhimu wa kulijadili kwa kina suala,hilo.
Kutokana
na hali hiyo Lowassa amewatahadharisha viongozi wa vijiji kuhakikisha
waiondoa kero hiyo, kabla ya uchaguzi ujayo wa serikali za mitaa
vinginevyo tatizo hilo litawagharimu.
Aidha Mh
Lowassa ambaye yeye pamoja na mbunge wa Viti maalum Namelok Sokoine
ndiyo waliyoiandaa semina hiyo, amempongeza mbunge wa zamani wa Monduli
hayati Edward Moringe Sokoine, kwa kufanikisha makubaliano kati ya
wilaya na jeshi kuhusiana na matumizi ya ardhi.
"Marehemu
Sokoine alifanya jambo kubwa sana kwa kufikia makubaliano yale na faida
yake kwetu sisi wana Monduli ni kubwa kimejengwa Hapa Chuo kikubwa cha
kijeshi(TMA), na tulikubaliana tusilipwe fidia na jeshi ili tuwe na haki
kwa mifugo yetu kuingia eneo lile,lakini kuna watu wameipeleka
halmashauri mahakamani kupinga" alisema na kuonya kuwa" tutapambana
kuhakikisha tunashinda! tumekuwa na mahusiano mazuri na jeshi na
tunataka mahusiano hayo yaendelee".
Naye
mbunge wa viti maalum Nameloki Sokoine alisema kuwa madhumuni ya kuandaa
semina hiyo ni kutoa dira itakayofafanua nini kifanyike kuondoa tatizo
hilo la uuzaji holela wa ardhi.
Amesema
mifugo na binaadamu wamekuwa wakiongezeka lakini ardhi ni ile ile kwa
hivyo bila ya kuwepo kwa dira na mipango thabiti hali itakuwa mbaya.
Aidha
alitoa changamoto kwa mbunge wa Monduli Mh Lowassa kusaidia kupatikana
kwa wawekezaji wa viwanda vya maziwa, ngozi na nyama wilayani Monduli.
"Ningependa
kumuomba Mh mbunge najua hili analiweza atusaidie watu wa Monduli
tupate wawekezaji wa viwanda vya ngozi, maziwa na nyama,tukiwa na
viwanda hivi itasaidia wafugaji kuachana na ufugaji wa kimila wa ng'ombe
wengi an badala yake kuwa na ng'ombe wachache wa kisasa wenye tija"
alisema Namelok na kushangiliwa.
Post a Comment