Mshindi
wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu huenda akavuliwa taji
hilo kama serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo na Baraza lake la Sanaa la Taifa ambalo ndio watoaji vibali vya
mashindanio hayo na kusimamia dhima na maudhui ya shindano hilo pamoja
na kusimamia maadili yake itaingilia kati
moja kwa moja suala hilo kwa kuunda tume maalum ya kulichunguza na
kutafuta ukweli halisi wa umri wa mrembo huyo na kutoa mapendekezo ya
ama Sitti avuliwe taji hilo na kuvikwa Mshindi wa pili, Lillian Kamazima
(pichani kulia) ama vinginevyo.
Kushoto ni Jihhan Dimachk aliyeshika nafasi ya tatu.
Shindano
la Miss Tanzania 2014 lilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City,jijini
Dar es Salaam Oktoba 11, na Sitti Mtemvu kuvikwa taji hilo na kuanza
utata wa umri wake halisi licha ya kuanika hadharani cheti chake cha
kuzaliwa ambacho wadau wa sanaa ya urembo kukitilia shaka na kushindwa
kuoanisha na pasi yake ya kusafiria na leseni ya udereva iliyotolewa
nchini Marekani.
Post a Comment