PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HABARI ZA HIVI PUNDE: CHIDI BENZ AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA UWANJA WA NDEGE WA DARESALAAM
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jij...


 
Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini Mbeya kwenye show ya Instagram Party inayotarajiwa kufanyika kesho.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo msanii Shetta ambaye alikuwa naye pamoja katika safari hiyo ya kuelekea Mbaya, amethibitisha kukamatwa na kwa Chidi akiwa na vitu vinavyohisiwa ni madawa ya kulevya.


“Kweli tulipata matatizo na Chidi pale airport ila mimi nikaruhusiwa yeye nikamuacha, amekamatwa na mambo mambo fulani sema ongea na wahusika watakwambia zaidi,” alisema Shetta.


Akizungumza na Millard Ayo, kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani kamanda wa polisi katika uwanja wa ndege Dar es Salaam amesema Chidi Benz amekiri kuwa dawa hizo ni zake.
Amedai kuwa Chidi alikutwa na kete 14 za dawa za kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi iliyokuwa mifukoni mwake.


Chidi atapandishwa mahakamani hivi karibuni kwa kosa la kukutwa na dawa hizo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top