Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Kutokana na ufinyu wa nafasi za
ajira serikalini na katika sekta binafsi iko haja ya vijana kuwa na
ndoto za kujiajiri pindi wanapokuwa vyuoni ili kupunguza tatizo sugu la ajira
ukosefu wa ajira unaoikabili Tanzania na dunia kwa ujumla.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema anashauri vijana kuwa na ndoto za
kujiajiri kwa kutumia vipaji na uwezo walionao kujiajiri badala ya kusubiria
kuajiriwa.
Lema anaeleza kuwa tatizo la ajira ni kubwa kwa wastani vijana 100
wanaohitimu elimu ya chuo 20 wanapata
ajira na 80 wanabaki mitaani bila ajira .
Anashauri kuwa katika hali hiyo ni vyema vijana wakawa na fikra mbadala za
kujiajiri ili waweze kujikwamua kimaisha na kuondokana na umasikini.
Lema anawataka vijana kuwa na mawazo ya ubunifu kuungana kwa pamoja na
kuanzisha miradi ambayo itawasaidia na kuwaajiri vijana wenzao wasio na ajira.
Godbless Lema akitoa nasaha kwa wahitimu wa chuo cha ufundi na mafunzo ya
ustadi Tumaini college iliyopo jijini Arusha ,Lema amewaasa wahitimu hao
kutambua hali ngumu ya maisha iliyopo
katika jamii inayowazunguka hivyo wajipange kwa jinsi ya kukabiliana nayo.
"Endapo mkihitimu chuo na kubahatika kupata nafasi za kazi bado
unatakiwa utamani kujiajiri na kuwaajiri
wengine " Alifafanua Lema
Mafanikio yanahitaji mtu kuwa na ndoto kama huna ndoto ni vigumu kufanikiwa
ni vizuri kila kijana awe na ndoto ambayo inamwongoza kwenye mafanikio.
"Chimbuko la utajiri na umasikini ukiweka na ndoto ukaweka juhudi na
nidhamu unaweza kufanikiwa cha msingi usikate tamaa" alisema Lema
Ukifikiri na kuamini kuwa unaweza
utaweza na ukiamini hauwezi hautaweza na hiyo ndio kanuni ni muhimu kuwa na
fikra chanya.
Huwa naamini katika kanuni moja kuwa Kila kinachoshindikana ni maamuzi
ya ndani ya mtu na kila kinachowezekana ni maamuzi ya ndani ya mtu
Vijana wawe na malengo ya muda mrefu si unaingia kazini januari inafika Aprili unataka uwe na gari unajikuta
unaingia kwenye vishawishi vikubwa sana.
Amewataka wahitimu hao waingie mitaani wakiwa na mawazo ya kufanya kazi kwa
kutumia vipaji,uwezo na uelewa walionao .
Vijana watulie kwenye ndoto zao waangalie namna ya kuzitimiza ,wadumu
katika nidhamu wasikimbizane na fashion badala yake wajiwekee akiba .
Mkuu wa Chuo cha Tumaini college Ernest
amesema kuwa chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo mbali mbali katika fani
za ualimu,utalii na hotelia ujuzi ambao umekua ukiwasaidia kuajiriwa na
kujiajiri wenyewe pindi wanapohitimu.
Wiliam Msofe ni Mhitimu wa chuo hicho amesema kuwa changamoto kubwa
inayowakwamisha vijana kujiajiri ni mitaji hiyo ameziomba tasisi za fedha
kuweka mfumo rafiki utakaowawezesha vijana kukopesheka na kujikwamua kiuchumi.
0765938008
Post a Comment