PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: GODBLESS LEMA AWATAKA VIJANA NCHINI KUWA NA NDOTO ZA KUJIAJIRI BADALA YA KUSUBIRIA KUAJIRIWA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. Kutokana na ufinyu wa nafasi za   ajira serikalini na katika sekta binafsi iko haja ya vijana kuwa ...



Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Kutokana na ufinyu wa nafasi za  ajira serikalini na katika sekta binafsi iko haja ya vijana kuwa na ndoto za kujiajiri pindi wanapokuwa vyuoni ili kupunguza tatizo sugu la ajira ukosefu wa ajira unaoikabili Tanzania na dunia kwa ujumla.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema anashauri vijana kuwa na ndoto za kujiajiri kwa kutumia vipaji na uwezo walionao kujiajiri badala ya kusubiria kuajiriwa.
Lema anaeleza kuwa tatizo la ajira ni kubwa kwa wastani vijana 100 wanaohitimu  elimu ya chuo 20 wanapata ajira na 80 wanabaki mitaani bila ajira .
Anashauri kuwa katika hali hiyo ni vyema vijana wakawa na fikra mbadala za kujiajiri ili waweze kujikwamua kimaisha na kuondokana na umasikini.
Lema anawataka vijana kuwa na mawazo ya ubunifu kuungana kwa pamoja na kuanzisha miradi ambayo itawasaidia na kuwaajiri vijana wenzao wasio na ajira.
Godbless Lema akitoa nasaha kwa wahitimu wa chuo cha ufundi na mafunzo ya ustadi Tumaini college iliyopo jijini Arusha ,Lema amewaasa wahitimu hao kutambua  hali ngumu ya maisha iliyopo katika jamii inayowazunguka hivyo wajipange kwa jinsi ya kukabiliana nayo.
"Endapo mkihitimu chuo na kubahatika kupata nafasi za kazi bado unatakiwa  utamani kujiajiri na kuwaajiri wengine " Alifafanua Lema
Mafanikio yanahitaji mtu kuwa na ndoto kama huna ndoto ni vigumu kufanikiwa ni vizuri kila kijana awe na ndoto ambayo inamwongoza kwenye mafanikio.
"Chimbuko la utajiri na umasikini ukiweka na ndoto ukaweka juhudi na nidhamu unaweza kufanikiwa cha msingi usikate tamaa" alisema Lema
Ukifikiri na kuamini  kuwa unaweza utaweza na ukiamini hauwezi hautaweza na hiyo ndio kanuni ni muhimu kuwa na fikra chanya.
Huwa naamini katika kanuni moja kuwa Kila kinachoshindikana ni maamuzi ya ndani ya mtu na kila kinachowezekana ni maamuzi ya ndani ya mtu
Vijana wawe na malengo ya muda mrefu si unaingia kazini januari  inafika Aprili unataka uwe na gari unajikuta unaingia kwenye vishawishi vikubwa sana.
Amewataka wahitimu hao waingie mitaani wakiwa na mawazo ya kufanya kazi kwa kutumia vipaji,uwezo na uelewa walionao .
Vijana watulie kwenye ndoto zao waangalie namna ya kuzitimiza ,wadumu katika nidhamu wasikimbizane na fashion badala yake wajiwekee akiba  .
Mkuu wa Chuo cha Tumaini college Ernest  amesema kuwa chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo mbali mbali katika fani za ualimu,utalii na hotelia ujuzi ambao umekua ukiwasaidia kuajiriwa na kujiajiri wenyewe pindi wanapohitimu.
Wiliam Msofe ni Mhitimu wa chuo hicho amesema kuwa changamoto kubwa inayowakwamisha vijana kujiajiri ni mitaji hiyo ameziomba tasisi za fedha kuweka mfumo rafiki utakaowawezesha vijana kukopesheka na kujikwamua kiuchumi.
0765938008

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top