PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Bilionea wa Lake Oil aendeleza unyanyasaji kwa wafanyakazi wake
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  SAKATA la mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lake Oil ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, Ally Edha Awadhi, kuwanyanyasa, kuwafukuza ka...
 


SAKATA la mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lake Oil ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, Ally Edha Awadhi, kuwanyanyasa, kuwafukuza kazi na kutumia mabaunsa wake kuwafanyia vitendo vya kikatili wafanyakazi wake linaendelea kufukuta ndani ya kampuni hiyo baada ya mfanyakazi mwingine kufanyiwa unyama na mwajiri huyo kisha kuachishwa kazi kiaina.

Awadhi anayetajwa kama mmoja wa mabilionea vijana nchini, mara kadhaa amefunguliwa mashitaka Polisi ya kuteka, kudhalilisha wafanyakazi wake kinyume cha maumbile na kupora mali zao bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

Imeelezwa kuwa mmiliki huyo amekuwa na ubavu wa kunyanyasa wafanyakazi wake katika kipindi kirefu ambapo licha ya walalamikaji kutoa taarifa katika vyombo vya dola bado kasumba ya kunyanyasa wafanyakazi wake bado anaendelea navyo bila kuogopa mkono wa sheria.



Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo ambaye alipata ajali kazini Desemba mwaka jana akiwa katika mkoa wa Shinyanga na kupewa kiasi cha shilingi 250,000 tu kama malipo ya kuumia kazini

Taarifa za kuaminika  zinaeleza kuwa Juni, 2013 mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo (jina tunalo) alihamishiwa kikazi katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kutoka katika kituo alichokuwa akifanyia mwanzoni (makao makuu ya kampuni hiyo) kabla ya kuachishwa kazi kwa sababu zisizojulikana.

Aidha, imeelezwa kuwa mlalamikaji huyo mwenye umri wa miaka 44 tangu alipohamishwa mkoa wa Shinyanga ilikuwa njia ya kuachishwa kazi na amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa (Ally) na kumfanya aishi kwa wasiwasi licha ya kuishi katika mazingira magumu kikazi. Katika kipindi chote alichofanya kazi katika kampuni hiyo aliteswa na polisi wanaodaiwa kupewa fedha kama kishawishi cha kutekeleza azma hiyo (rushwa) na mwajiri huyo.

Kwa upande wake mlalamikaji huyo amesema baada ya tukio hilo alifuatilia fedha zilizoamriwa na OSHA kuwa apewe kwa zaidi ya miezi mitatu bila mafanikio.

“Baada ya kuhamia Kahama tulienda kikazi Mwanza tukapata ajali gari ya kampuni iligongwa kwa nyuma, tuliumia watu wawili na tulipofuata taratibu zote, Wakala wa Usalama wa Afya Mahali pa Kazi (OSHA), aliiamuru Kampuni inilipe (mlalamikaji) milioni 32 lakini hadi sasa mimi mwenyewe sijapatiwa hiyo fedha wala watu wa Bima hawajanipatia fedha zangu kwamaana kampuni ya Like Oil iliwasiliana na watu wa bima ili nilipwe fedha zangu”.



Mwonekano wa gari hilo lenye namba T 681 CHP mali ya kampuni hiyo baada ya kupata ajali jijini mwanza mapema mwezi Machi mwaka huu. Gari hilo lilikuwa na wafanyakazi wawili ambao waliumia vibaya



Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo amesema “Hii kampuni hata mimi nafanya hapa lakini inanyanyasa wafanyakazi wake kuna mtu aliyeumia kazini, Hamis Bakari, hajalipwa fedha ambazo zinamstahili kisheria bali alipewa shilingi 250,000 tu ambazo hata hakuweza kujibibu, hawakufikiria aliokoa tani 50 ya gesi iliyopo kwenye ghala na maisha ya wananchi wanaoishi karibu na eneo tunalofanyia kazi baada ya kutokea hitilafu ya kulipuka kwa gasi bali wanampa kiasi kama hiki na polisi wanashuhudia”

Barua kwa Waziri Mkuu

Hatua hiyo ilimfanya mlalamikaji kumuandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (FikraPevu imepata nakala) kuwa licha ya jitihada mbalimbali alizozifanya kwa ajili ya kupata angalau fidia ya ajali ambayo (OSHA) waliamuru kuwa alipwe na kwamba kesi yake ipo katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi huku akimweleza kuwa kesi hiyo ingesikilizwa Septemba 16, 2014 ambapo sasa imeahirishwa tena baada ya kufanyika kwa mashauriano hadi Octoba 13, 2014.

Barua hiyo imeeleza kuwa mlalamikaji aliwahi kubambikiziwa kesi ya kuisababishia hasara kamuni milioni 100, hali ambayo mlalamikaji alidai deni hilo halimhusu. Deni hilo lilisababishwa na kitengo ambacho yeye hakuhusika kwani mauzo aliyosimamia akiwa Shinyanga ni milioni 70 ambazo pia alituma ripoti iliyoambatana na stakabadhi ya mauzo aliyoyafanya (ushahidi upo).

“Nilisingiziwa madeni lakini nilimwambia mwajiri wangu mambo ya kiofisi (fedha za kampuni) sitashughulikia nikiwa Kahama (ushahidi ninao kwamaana alikubali kwa maandishi) pamoja na hilo mimi sikuruhusiwa kutoa mali yeyote bila idhini ya makao makuu Dar es Salaam hivyo pakiwa na uhitaji wa mzigo, Ofisi ya Dar es Salaam wanatuma Invoice na ndipo mzigo unatolewa” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Pia amemweleza Waziri Mkuu kuwa baada ya kufukuzwa kazi ameshindwa kumsomesha mtoto wake ili aweze kuendelea na masomo yake na kwamba amejaribumara kadhaa kumshawishi mwajiri wake kuwa ampatie haki yake lakini hakufanikiwa kupata haki yake hadi sasa na kuwa amemuomba aingilie kati suala hilo ilia pate haki yake.

FikraPevu imebaini kuwa licha ya Waziri Mkuu kuandikiwa barua, shauri hilo linaendelea kushughulikiwa katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ambapo mwenendo wa usuluhishi wa shauri hilo umetajwa mara mbili hadi sasa. Imeelezwa kuwa Mwanasheria wa kampuni hiyo, Siraiya Mafiah, Septemba 16, 2014 alishauri pande zote mbili kuwa suala hilo lisichukuliwe kwa mapana yake bali ataenda kuongea na mwajiri wake (Ally) ili aweze kutatua mgogoro huo haraka iwezekanavyo.

Mlalamikaji anaendelea kumweleza Waziri Mkuu kwamba kutokana na mateso makali na vitisho alivyopewa, aliwahi kupata ajali jijini Mwanza mwaka jana akiwa na gari la kampuni na kwamba hakupewa fedha za matibabu wala za kuhudumia familia yake wakati akiugua na kwamba alilazimika kutumia fedha za ada ya mtoto wake ambaye kwa sasa ameshindwa kuendelea na masomo.

Juhudi za kumtafuta Waziri Mkuu kupitia Msemaji wake zimekuwa zikiendelea bila mafanikio ili kujua hatima ya barua ya mlalamikaji, huku ikibainika kuwa kamuni hiyo haijawahi kutekeleza maagizo ya mamlaka zinazosimamia vifaa vya kuzima moto hadi kupelekea kampuni hiyo kulipishwa faini zaidi ya mara tatu katika vipindi tofauti.



Barua za Jeshi la Polisi, Kikosi cha Zima Moto mkoani Shinyanga katika Wilaya ya Kahama zikionyesha uthibitisho wa kulipishwa faini kampuni hiyo kwa kupuuza agizo la kujaza fomu maalumu kwa ajili ya ukaguzi wa kituo hicho cha kampuni hiyo kilichopo Shinyanga.



Kumbukumbu zinaonyesha kuwa katika tukio la hivi karibuni mmoja wa wafanyakazi hao alidai kupigwa, kudhulumiwa mali zake (yakiwemo magari) na mwajiri wake (Ally) na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, kabla hajaripoti katika Kituo cha Polisi Oysterbay Mei 2, 2013 na kisha kumwandikia barua ya malalamiko Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo pia alidai kuwa mwenendo wa kesi yake hauendi vizuri hali iliyomfanya Waziri Mkuu kuliagiza Jeshi hilo kufanyia kazi kesi hiyo.

credit fikra pevu

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top