PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WENJE ASEMA YUKO TAYARI KUGHARAMIA KIKAO CHA UKAWA ILI KUJA NA JINA MOJA LA MGOMBEA URAISI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  ...

 


Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje amesema yuko tayari kugharimia kikao Maalumu cha UKAWA,
"Nitagharimia kwa pesa zangu kikao cha viongozi wanaounda Umoja wa Katiba UKAWA nje ya nchi na kufikia msimamo wa kusimamisha mgombea mmoja."
Alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya Furahisha Mwanza mbele ya makamo wa Rais wa Zanzibar Maalim Self Sharrif Hamad.
Alisema kutokana na umuhimu huo yuko tayari kugharimia kikao cha wiki moja nje ya nchi kwa viongozi wa UKAWA kujifungia na kuwa na jina moja la mgombea wa Urais katika uchaguzi wa 2015.
Haiwezekani watanzani kuendelea kuwa masikini wakati kuna watalaamu kama Prof Ibrahim Lipumba hawapewi nafasi ya kujenga uchumi na wakati wenzetu wa mataifa mengine wanawatumia.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top