PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WANANCHI WA KWA MOROMBO WAMEASWA KUFANYA USAFI WA VYOO ILI KUEPUKA UGONJWA WA U.T.I
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA ELINIPA E. TEMBA   Wananchi wameaswa kuwa na desturi ya kufanya usafi wa vyoo ili kujiepusha na ugonjwa wa U.T.I ambao umekuwa ukiw...

NA ELINIPA E. TEMBA

 Wananchi wameaswa kuwa na desturi ya kufanya usafi wa vyoo ili kujiepusha na ugonjwa wa U.T.I ambao umekuwa ukiwapata akina mama  na watoto.


Hayo yamesemwa na daktari wa zahanati ya oljoro jijini arusha Dk. Ayubu mashack katika mahojiano na mwandishi wetu hapo jana ambapo amesema kuwa wanainchi wanatakiwa kuwa makini katika kuepuka swala la ugonjwa wa U.T.I kwa kufanya usafi katika vyoo kila siku

Dokta Ayubu Mashack akizungumza na mwandishi wetu Elinipa Temba katika kufahamisha umma kuhusu ugonjwa huu wa U.T.I  mapema jana.Picha na Selemani Juma Kodima

Dk Ayubu alisema kuwa ugonjwa wa U.T.I ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria icolay ambaye anasababisha urinary tract infection  kwenye njia ya uzazi
Licha ya Dk Ayubu kusema ni bacteria icolay aliweza kuzitaja dalili mbalimbali ambazo mwanajamii anapoziona anaweza kujua kama ameshapata ugonjwa huu wa U.T.I
“Dalili kubwa ni chief complain ambayo inapelekea maumivu makali wakati waaja ndogo  na wakati mwingine maumivu  chini ya kitovu ,homa kali hasa kwa watoto na wakati mwingine kichefuchefu kwa watu wazima na kukojoa mara kwa mara “alisema Dk Ayubu
Ugonjwa huu umekuwa ukiwashambulia sana wakina mama na watoto hali inayopeleke kuwa na wagonjwa wengi wenye kupata ugonjwa huu wa U.T.I ambao wamekuwa wakikumbwa na jangwa hili.
Dk Ayubu alisema yapo madhara ambayo mgonjwa wa ugonjwa huu asipoutilia matibabu akaweza kukumbwa na hali ya utasa,hali inayopelekea mwanamke kutoshika mimba hali inayopelekea wasiwasi kwa familia nyingi ambao hawapo makini na ugonjwa huu
DK .Ayubu akizunguma kwa kina zaidi kuhusu  dalili za ugonjwa huu wa U.T.I  
Picha na selemani juma kodima
Vilevile amesema kuwa zipo juhudi nyingi  ambazo zinafanywa ili kuwapa jamii elimu ya  kuhusu namna ya kuepukana naugonjwa huu na kuwapa uelewa mpana wa ugonjwa huu wa U.T.I  japo matibabu yapo kwa ugonjwa huu
Dk ayubu amewashauri kuwa wanajami kuwa makini iwapo tu wanapoona dalili za ugonjwa huu wa U.T.I ili kuepukana na madhara yanayotokana  ugonjwa huu
wanajamii wakiona dalili yoyote wawe wepesi kuja kwenye  vituo vya afya kwa ajili ya kupata matibabu ya ugonjwa huu wa U.T.I”Alisema Dk ayubu
credit: ruwenzoriclass blog

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top