Habari na KUNDAEL PHILLIP
Mkoa wa Arusha eneo la kwa murombo ni maarufu sana kwa biashara ya mbuzi kwa ajili ya matumizi ya nyama za kuchoma pamoja na supu.Biashara ya mbuzi ni maarufu sana kwa kabila la wamasai na hufanyika mara mbili kwa wiki katka soko la kwa murombo,siku ya Jumatatu na Ijumaa.
Bwana Richard Kivuyo ambaye ni mfanya biashara mkubwa na
mzoefu katika soko hilo la mbuzi alisema biashara hiyo inafaida kiasi kwani
hali ya uchumi kwa sasa ni ngumu ukilinganisha na kipindi cha nyuma kwani mbuzi
mmoja kwa sasa ni shilingi laki moja japo msimu wa sikukuu biashara huwa nzuri
kiasi unaweza ukauza kwa laki na hamsini elfu.
Biashara yetu mara nyingi tunafanyia hapahapa katika
eneo la kwa murombo japo sisi tunawatoa maeneo ya vijijini huko tunapoishi na
wateja wetu ni wa eneo hili japo wapo wanaotoka maeneo mengine ambao hununua
kwa jili ya kitoweo na kufuga.
Aliendelea kueleza kwamba biashara hii pia ina hasara na
ndio changamoto wanayokabiliana nayo inapotokea mbuzi kuumwa na kukosa tiba kwa
haraka,vilevile inapotokea mbuzi akiwa mjamzito kwani tuna mbuzi jike na dume
hivyo na unapofika mda wa kuzaa inaweza
kutokea mtoto akafa au wote kwa pamoja,na ukame pia huchangia kwani wakati
mwingine tunalazimika kununua majani kwa sababu hayaonekani kwa urahisi.
Aliomba serikali iweze kuwasaidia kujenge soko maalumu
katika eneo hili la kwa murombo kwa jili ya biashara hiyo kwani wanapofanyia
biashara yao kwa sasa mazingira yake ni magumu hinyo inapofika kipindi cha mvua
tope hujaa eneo hilo na biashara kuwa ngumu vilevile inapofika mda wa kiangazi
nao inakua kero kutokana na jua kua kali.
Huduma muhimu
kama vyoo hakuna eneo hili inatulazimu kutoa fedha na kwenda kwenye vyoo vya kulipia
ambavyo inakua vigumu wote kufanya hivyo nakua chanzo cha uchafuzi wa mazingira
kwani watu hujisaidia hovyo katka eneo hili.
‘Hakuna vyoo kabisa katika eneo hili la biashara nayo serikali ituangalie.’alisema bwana Richard kivuyo..
Post a Comment