Mkurugenzi
wa Habari, Elimu kwa Umma na Itifaki wa Bunge Maalum la Katiba, Bw.
Jossey Mwakasyuka (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa semina
iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari kuhusu kuimarisha
Uandishi wa Habari za shughuli za Bunge iliyofanyika tarehe 6 Septemba,
2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma. Kulia ni
Mshauri wa mambo ya Kiufundi toka Shirika la UNDP, Bi. Anna
Kochannesyan.
Mhariri
Mtendaji Jamhuri Media Limited, Bw. Deodatus Balile akitoa mada mbele
ya waandishi wa habari (hawako pichani) inayohusu Athari za Siasa katika
uandishi wa Habari za Bunge, Madhara ya Vyombo vya habari kutumika,
Miiko na Maadili ya kuzingatia wakati wa semina kwa ajili ya waandishi
wa habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African
Dreams Conference mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Kamati za Bunge Maalum, Bw. Athumani Hussein akitoa
mada inayohusu Uandishi wa habari za Bunge na Siasa wenye tija kwa Taifa
wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari
iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams
Conference mjini Dodoma.
Mshauri
wa mambo ya Kiufundi toka Shirika la UNDP, Bi. Anna Kochannesyan
akichangia mada wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa
habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African
Dreams Conference mjini Dodoma.
Afisa
Habari wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Owen Mwandumbya akifafanua jambo
wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari
iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari iliyofanyika tarehe 6
Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini mada zikizowasilishwa
wakati wa semina iliyoandaliwa leo kwa ajili yao iliyofanyika tarehe 6
Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
Na Magreth Kinabo, Maelezo.
WAANDISHI
wa habari nchini wameaaswa kuandika habari zinazohusiana na masuala ya
Bunge, likiwemo Bunge Maalum la Katiba kwa kuzingatia weledi na
kujiepusha kuwa na maslahi binasfi au ya kisiasa.
Hayo
yalisemwa leo 6 Septemba, 2014 na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri ,
Deodatus Balile wakati wa semina kuhusu namna bora ya kuimarisha
uandishi wa habari za shughuli za Bunge iliyofanyika kwenye hoteli ya
African Dreams mjini Dodoma.
Akizungumza
awali kabla ya kuanza kwa Semina hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Habari
ya Bunge kwa kushirikana na Shirika la UNDP, Mkurugenzi wa Habari,
Elimu kwa Umma na Itifaki wa Bunge Maalum, Bw. Jossey Mwakasyuka
amesema lengo lake ni kuweza kujadiliana na kubadilishana uzoefu juu
ya uandishi wa habari hizo kwa waandishi hao ili kuweza kuandika habari
sahihi.
Balile
amesema hayo wakati akitoa mada kuhus u Athari za kisiasa katika
uandishi wa habari wa Bunge , Madhara ya Vyombo vya Habari kutumika,
miiko na maadili ya kuzingatia kwenye uandishi wa habari hizo.
“Ni
lazima kutenganisha uandishi wa habari na siasa, ikiwa kama unataka
kuingia katika siasa basi inapaswa kuacha kazi ya uandishi wa habari,”
alisema Balile.
Aidha,
Balile amewataka waandishi wa habari kujiepusha kuandika habari
zinazohusu siasa na Bunge ambazo zinajenga chuki katika jamii, ikiwemo
kuiingiza hisia binafsi ama upendeleo.
“Ni
vema habari zinazohusu maendeleo, umoja mshikamano na zenye kuleta
amani zipewe kipaumbele,” alisisitiza Balile.
Aliongeza kuwa ni vema waandishi hao wakajenga tabia ya kujiendeleza
kielimu katika fani mbalimbali ili kuweza kufanya kazi hiyo kiufasaha na
kujiheshimu kwani wakijiheshimu nao wataheshimiwa,huku akiwapongeza
baadhi yao ambao wamejiendeleza au wanajiendeleza kielimu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Kamati za Bunge Maalum, Athuman
Hussein, akitoa mada kuhusu Uandishi wa Habari za Kibunge wenye Tija
kwa Taifa amewataka waandishi hao kuweza kukumbuka mara kwa mara mambo
ambayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika kazi zao.
“Unapoandika
habari za Bunge ni lazima uwe na uelewa wa matarajio ya wananchi ili
uweze kuandika habari zenye tija. Huwezi kuandika habari zenye tija
kama hujui matarajio ya wananchi,” alisema Hussein.
Hussein aliongeza kuwa na uelewa juu ya Bunge na majukumu yake, muundo wake na mifumo yake ni jambo muhimu kwa waandishi.
Post a Comment