PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: UCHAFU KATIKA SOKO LA MBAUDA WAWAKERA WAFANYABIASHARA KATIKA SOKO HILO.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Hali isivyo ya kuridhisha katika soko la mbauda lililoko mkoani Arusha katika kata ya sombetini kutokana na kutapakaa kwa u...


 Hali isivyo ya kuridhisha katika soko la mbauda lililoko mkoani Arusha katika kata ya sombetini kutokana na kutapakaa kwa uchafu.   picha na Rosemery Mmbando.

          
  Wafanya biashara katika soko la Mbauda mkoani Arusha wameulalamikia uongozi wa kata ya sombetini lilipo soko hilo juu ya uchafu unaoletwa na wakazi wa jirani na soko hilo.
Akizungumza na muandishi wa habari hizi mmoja wa wafanyabiashara hao Bwana Mikaeli Materu amesema kuwa uchafu wa soko hilo unachangiwa na majirani wa soko hilo kuleta takataka kutoka majumbani mwao.

                 Bwana Mikaeli Materu akitoa maelezo wakati akizungumza na muandishi wa habari sokoni                    hapo . Picha na Rosemery Mmbando.

Bwana Materu ambaye ni mfanya biashara wa sokoni hapo tangu miaka ya 1990 amesema uchafu kama nywele na ngozi za wanyama ni uchafu usiozalishwa sokoni hapo lakini utaukuta katika mazingira ya soko hilo.
Akibainisha changamoto nyingingine bwana Materu amesema ukosefu wa mtaro wa maji taka sokoni hapo ni kero ambayo inawasumbua na hujitokeza zaidi katika kipindi cha mvua.
Pamoja na kuwa na kero hizo Bwana Materu amesema licha ya wenyeji na uzoefu alionao sokoni hapo hatambui kama kuna uongozi wa soko au lah.

                        Mpangilio mbovu wa wafanya biashara na mazingira machafu katika soko la mbauda                                       mkoani Arusha.  Picha na Rosemery Mmbando. 

Juhudi za kumpata diwani wa kata ya sombetini Bwana Ally Bananga hazikufanikiwa kutokana na kutokuwepo katika ofisi ya kata hiyo.Bwana Materu alimaliza kwa kuuomba uongozi wa kata hiyo na halmashauri kuboresha mazingira ya soko ili kupunguza msongamano wa wafanya biashara katikati ya jiji la Arusha.

                 Biashara zikiendelea sokoni hapo bila ya kujali hali ya usafi wa mazingira yenyewe.  .

Soko la Mbauda katika kata ya Sombetini mkoani Arusha si soko rasmi lakini hata hivyo limekua msaada mkubwa kwa wakazi wa kata hiyo na maeneo ya jirani.

  Habari na; Eliamini Mchome na Rosemery Mmbando.
chanzo: AJTCTV BLOG

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top