Sitta aliwafananisha viongozi wa Ukawa na wasanii waigizaji, akitabiri kuwa watashindwa vibaya katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Halikadhalika, mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo ‘kuwapoza’ wajumbe ambao ni waumini wa Dini ya Kiislamu wanaopaza sauti wakitaka Mahakama ya Kadhi itambuliwe, akisema kuna ‘namna’ itaingizwa kwenye Katiba.
Sitta alitoa matamko hayo mawili jana, wakati akiendesha vikao vya Bunge hilo mjini Dodoma, katika kipindi ambacho suala la Mahakama ya Kadhi likiwa limewagawa wajumbe wa Bunge hilo katika makundi mawili kwa misingi ya imani za dini zao.
Alianza kwa suala la wasomi mbalimbali wanaohoji uhalali wa Bunge hilo kutaka kuruhusu wajumbe wake watakaokuwa nje ya nchi, kupiga kura ya uamuzi kupitisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa akisema:
“Kuna watu wanaojiita wasomi, nadhani wanaohusiana na hao wanaoitwa Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ambao jitihada yao kubwa sana ni kuzuia kabisa isipatikane katiba.” Sitta akaongeza kusema, “Leo (jana) nimemsikia mmoja anasema kwamba kupiga kura (nje) itakuwa sivyo tutakuwa tanavunja katiba ya nchi. Huyu mtu kasoma sheria ya uchaguzi,” alisema
Post a Comment