Arusha.
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), zinatarajiwa
kukutana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati ya upatikanaji wa umeme
wa uhakika kwa bei nafuu kupitia nishati mbadala.
Mkutano
huo ulioandaliwa na EAC kwa kushirikiana na Baraza la Biashara la
Afrika Mashariki (EABC), utafanyika Oktoba 31hadi Novemba Mosi, mwaka
huu ambapo wafanyabiashara wa nishati mbadala watapata fursa ya
kuonyesha huduma na bidhaa zao.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa EABC, Jonne Bruecher aliwambia waandishi wa
habari jijini Arusha jana kuwa mkutano huo utahudhuriwa na watu zaidi
200 wakiwemo viongozi wa Serikali, Wataalamu, Wafanyabiashara na wadau
wa sekta ya nishati mbadala.
“Nishati
ya uhakika na nafuu ni nyenzo muhimu katika juhudi za nchi wanachama wa
EAC kujikwamua kiuchumi. Lazima pawepo mbinu na mikakati ya pamoja
katika upatikanaji na matumizi ya nishati mbadala kwenye Ukanda huu wa
EAC,” alisema Bruecher ambaye ni Meneja maendeleo ya biashara wa EACB.
Utafiti
wa EABC kuhusu matumizi ya nishati kwa nchi za EAC inaonyesha kuwa
Kenya na Rwanda ndizo zinaongoza kwa kusambaza umeme kwa asilima 28 ya
wananchi wake, Tanzania ni ya tatu kwa asilimia 19, Uganda asilimia 16
wakati Burundi ni asilimia nne pekee.
Kwa
upande wake, Mshauri wa Sera na Utafiti wa EABC, Michael Baingana
alisema matumizi ya nishati mbadala utaongeza kiwango cha matumizi ya
nishati ya umeme kwa wananchi wa EAC, hasa vijijini ambao ni asilimia 80
ya raia wote wa EAC wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 140 milioni.
“Hadi
sasa ni asilimia ndogo tu ya wakazi wa EAC wenye kufikiwa na huduma ya
nishati ya umeme, nah ii ni moja kati ya changamoto zinazotukabili
katika harakati za kujiletea maendeleo,” alisema Baingana.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi
Mtendaji wa EABC, Andrew Luzze alisema ni muda muafaka kwa nchi za EAC
kutumia fursa ya upatikanaji wa jua na upepe wa ukakika kuzalisha umeme
mbadala badala ya kuendelea kutegemea vyanzo vingine kama maji, mafuta
na gesi ambavyo ni ghali.
Luzze
alisema matumizi ya nishati mbadala siyo tu itawahakikishia raia wa EAC
uhakika wa umeme, bali pia utapunguza bei ya bidhaa na huduma kutokana
na gharama nafuu ya uzalishaji.
Post a Comment