Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akifafanua jambo juu ya
kukabiliana na uharibifu wa vyanzo vya maji mara baada ya zoezi la
kubomoa nyumba zilizojengwa kwenye vyanzo liliofanywa na vijana wa
vijiji vya Olkung’wado,Uvizo ,Ngabobo na Ngarinanyuki ikiwa ni njia ya kutunza bonde dogo la mto Ngarinanyuki.Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mbunge wa
Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari amesema kuwa watu wote wanaoharibu
vyanzo vya maji katika jimbo hilo hawatasalimika lazima wachukuliwe hatua kali
bila kujali wadhifa wao ili kulinda vyanzo hivyo kwa ajili ya upatikanaji
endelevu wa maji.
Kufuatia
zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa kwenye vyanzo vya maji vya Inteki kilichoko kijiji cha Kireeni lililofanywa na vijana wa jamii ya Wameru kutoka vijiji vya
Olkung’wado,Uvizo ,Ngabobo na Ngarinanyuki .
Mbunge huyo
amewapongeza vijana hao kwa kazi
waliyoifanya kwa kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vinalindwa kwa gharama
yeyote ile .
‘Nawaunga
mkono vijana kwa kazi mliyoifanya niseme kuwa yeyote anayeharibu vyanzo vya
maji hatasalimika lazima tumchukulie hatua haijalishi nani yuko nyuma yake awe
kiongozi au yeyote yule kwasababu maji ni muhimu kuliko maisha ya mtu yeyote Yule”
Alisema Nassari
Pia Mbunge
huyo ameahidi kuchangia miti kwa ajili ya zoezi la upandaji miti katika vyanzo
vilivyoharibiwa na watu.
Kwa upande
wao wananchi wameeleza kuwa wamefanya zoezi hilo baada ya kuona serikali
imeshindwa kulinda vyanzo hivyo kutokana na baadhi ya watu ambao hufanya
shughuli za kilimo katika vyanzo hivyo na wanapokamatwa huachiwa na kurudi
uraiani bila kuchukuliwa hatua za kisheria.
Steven John mwananchi wa kata hiyo amesema kuwa Mgogoro
huo ulidumu kwa muda mrefu na kukosa suluhu hivyo wananchi wameamua kuchukua
hatua ili kunusuru vyanzo hivyo kwasababu wao ni waathirika wakubwa.
Mwanakijiji Frank
Nko amesema kuwa uharibifu huo
umekithiri kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hatua ya kuingilia kati baada ya
kuona kuwa serikali imeshindwa kudhibiti.
Mwenyekiti
wa jumuiya ya maji bonde dogo la Ngarinanyuki ,Aminieli Mungure amesema kuwa vyanzo hivyo vimekua vikiharibiwa a kukosa
usimamizi hivyo wakati umefika wa jamii kuamka na kuvilinda .
“Bonde dogo
la Ngarinanyuki linalisha maji safi na kumwagilia vijiji zaidi ya vinne ambavyo
ni Olkung’wado,Uvizo ,Ngabobo na Ngarinanyuki uharibifu ni mkubwa kwa hatua
zinazochukuliwa ikiwemo kupanda miti tunaamini uzalishaji wa maji utaongezeka
na kutokua pungufu kama ilivyo sasa ” Alisema Mungure
Cecilia Lema
kutoka Ofisi ya Bonde la Kati Arusha amesema kuwa vyanzo vya maji vilivamiwa na
wanakiji waliamua kuyaondoa mazao hayo na kupanda miti na kuongeza kuwa kulinda vyanzo hivyo ni kutekeleza sheria
namba 7 ya maji.
|
Post a Comment