Sehemu ya CD Feki zilizokamatwa.
Msama akionesha CD zilizokamatwa katika maeneo ya Kariakoo na Kimara Bonyokwa.
Baadhi ya vifaa vinavyotumika katika kutengeneza CD feki zikiwa Kituo cha Polisi Urafiki.
Hizi ni sehemu ya CD feki zilizokamatwa.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akionyesha mashine ya kisasa
aina ya LG iliyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa kurudufu kazi za
wasanii (CD FEKI) katika maeneo ya Kariakoo na Kimarta Bonyokwa jijini
Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akionesha mashine ya kisasa
aina ya LG waliyokamatwa nayo watuhumiwa wa kurudufu CD feki za kazi za
wasanii katika maeneo ya Kariakoo na Kimara Bonyokwa jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP, Denis Moyo. (Picha na
Francis Dande)
Msama akionyesha wino na vifaa vingine vinavyotumika katika kutengeneza CD feki za kazi za wasanii.
Msama akionesha mashine ya kuprint Cover za CD.
CD feki zilizokamatwa katika maeneo ya Kariakoo.
Msama akizungumza na waandishi wa habari leo.
Lundo la CD feki zilizokamatwa katika maeneo ya Kimara na Kariakoo.
Kasha la CD iliyokuwa na nyimbo za mwimbaji Bahati Bukuku ikiwa imewekea stika feki ya TRA.
Baadhi ya CD feki zilizokamatwa na Kampuni ya Msama Auoctions Mart.
NA FRANCIS DANDE
OPERESHENI
ya kukamata watuhumiwa wa wizi wa kazi za wasanii, imeshika kasi baada
ya Kampuni ya Msama Auction Mart kukamata mashine za kisasa za kurudufu
kazi za wasanii na CD feki zenye thamani ya shs. milioni 200.
Huo ni
mkakati wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Vijana
Utamaduni na Michezo pamoja na Jeshi la Polisi katika vita ya
kuwapigania wasanii waweze kunufaika na kazi zao.
Mbali ya
wasanii, pia harakati hizo zinalenga kuiwezesha serikali kupata mapato
yake kutoka kwa wasanii ambao siku zote wamebaki duni huku wajanja
wachache wakivuna mamilioni ya fedha.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya
Msama Promotions, Alex Msama alisema operesheni hiyo ilifanyika mwishoni
mwa wiki katika maeneo ya Kariaakoo na Kimara Bonyokwa jijini Dar es
Salaam.
“
Ttumekamata vijana watano ambao wapo katika kituo cha Polisi cha Urafiki
na taratibu za kuwafikisha mahakamani zinafanyika,” alisema Msama.
Aidha,
Msama amesema katika zoezi hilo wanamshikiria mmiliki wa nyumba moja
ambayo baadhi ya watuhumiwa walikutwa wakifanya uharamia wa kudurufu
kazi za wasanii, hivyo kuikosesha serikali mapato yake halali.
“Kwa
namna hii, serikali haiewezi kupata mapato na pia wasanii wataendelea
kuwa ombaomba kutokana na kuibiwa kazi zao,” alisema Msama.
Msama
alisema, zoezi hilo ni endelevu na litafanyika nchi nzima ambapo kampuni
Msama kwa kushirikiana na Polisi wa Kituo cha Urafiki, wameweza
kuwakamata jumla ya watuhumiwa 20 ambao wanasubiri taratibu za kisheria
ili kesi zao ziweze kufikishwa mahakamani.
Msama
aliongeza, matunda ya operesheni hiyo, yameanza kuonekana kwani kwa
kushirikiana na raia wema, wameweza kukamata mashine moja kubwa ya
kisasa aina ya LG ambayo huweza kuzalisha CD feki zaidi ya ishirini kwa
dakika tano.
“Katika
kipindi kicha wiki moja tumekamata mzigo mkubwa wa shs mil.200 katika
maeneo ya Kimara Bonyokwa na Kariakoo na kazi bado inaenedelea,” alisma
Msama.
Msama
aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini,
amejitwika jukumu hilo zito katika kupigania maslahi ya wahusika ambao
wameshindwa kupiga hatua kutokana na wiki wa kazi zao.
Post a Comment