PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: LIGI KUU TANZANIA BARA YAWA NA MVUTO ZAIDI AFRIKA MASHARIKI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Wiki iliyoisha juzi imeshuhudia kuanza rasmi kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo ndiyo ya juu katika ngazi ya vilabu hapa nchini. Mwanzo ...
 


Wiki iliyoisha juzi imeshuhudia kuanza rasmi kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo ndiyo ya juu katika ngazi ya vilabu hapa nchini. Mwanzo huo ulikuwa na matokeo tofauti, yaliyotarajiwa na ambayo hayakutarajiwa.

Kwa Ufupi

Gumzo kubwa lilikuwa ni kupoteza mchezo wa ufunguzi kwa timu ya Yanga Afrika mbele ya Mtibwa Sukari Uwanjani Jamhuri, Morogoro.

Yanga, ilipoteza mchezo huo huku washabiki wake wakiwa na matarajio makubwa hasa baada ya ushindi mnono wa goli 3-0 dhidi ya Azam katika Ngao ya Hisani.

Ndanda FC ndio wanaongoza ligi kwa sasa, wakiwa kufuatia ushindi mnono wa goli 4-1 waliovuna uwanjani Kambarage walipocheza na wageni wenzao katika ligi, timu ya Stendi United ya Shinyanga.

Mabingwa watetezi, Azam FC waliibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Polisi Morogoro, timu iliyopanda daraja msimu huu katika mchezo ambao ulichezwa katika Uwanja wa Azam Complex.

Katika mechi zingine zilizochezwa Jumamosi, washindi wa tatu wa msimu uliopita, Mbeya City walitoka sare tasa (bila kufungana) na JKT Ruvu mkoani Mbeya, Tanzania Prisons wakapata ushindi wa 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.

Matokeo ya kushangaza yalikuwa mkoani Tanga ambako timu iliyonusurika kushuka daraja msimu uliopita, Mgambo Shooting, alivuna ushindi mwembamba a 1-0 dhidi ya Kagera Sugar uwanjani Mkwakwani, Tanga.

Vigogo wengine, Simba ya Dar es Salaam ilijikuta ikilazimishwa sare ya 2-2 mbele ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo uliochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Matokeo haya yalikuwa ya kushangaza kwa Simba kwani hadi kufikia mapumziko, tayari walikuwa wakiongoza 2-0.

Habari ya Ndanda kuongoza Ligi haipewi nafasi sana kwenye vyombo vya habari, kama vile tu ambavyo kushinda kwa Mtibwa kunafunikwa na taarifa za Yanga kufungwa.

Mtazamo wa Kiufundi

Matokeo ya wiki iliyopita yanaweza kuashiria Ligi yenye ushindani msimu huu, kwani tumeshuhudia timu ambazo sio kubwa zikipata ushindi katika raundi ya kwanza ya ligi.

Kwa kiasi fulani mwanzo wa Ligi ulikuwa kinyume na matarajio ya washabiki nguli ambao waliaminishwa kuwa timu zao ni bora kutokana usajili waliofanya.

Magazeti hayakukauka habari za usajili wa wachezaji wa kimataifa kutoka Brazil, Gerson Santos ‘Jaja’ na Andrey Coutinho ambao walisajiliwa na klabu ya Yanga. Kwa upande mwingine nao uhamisho wa Emmanuel Okwi kutoka Yanga kwenda Simba, pamoja na utata wake viliongeza mhemko wa washabiki wa Simba juu ya uchezaji wa kiungo huyo wa muda mrefu ktika soka la Bongo.

Sio kusema kuwa timu hizi zilicheza vibaya mechi zake za raundi ya kwanza, lakini maandalizi ya timu zingine yalipuuzwa. Timu ambazo sio Simba wala Yanga zilimlikwa kwa uchache sana na vyombo vya habari, na pengine ndio sababu ya matokeo ya wikiendi kushtusha wengi.

Kwa wafuasi wa mabadiliko, huu ni mwanzo mzuri kwani ni dalili ya Ligi ambayo itakuwa na ushindani. Kwa sasa Ndanda FC inaongoza ligi ikiwa na alama 3, ikifuatiwa na Azam, kisha Mtibwa na Prisons zote zikiwa na alama tatu kila moja lakini zikitofautishwa na idadi ya magoli.

Changamoto ya tiketi za Elektroniki

Baada ya majaribio katika mechi za maandalizi ya msimu wa Ligi, tiketi za elektroniki zilianza kutumika rasmo katika Ligi Kuu ya Vodacom. Mechi zote, isipokuwa mchezo kati ya Ruvu Shooting na Prisons katika Uwanja wa Mabatini ilitumia tiketi hizi.

Changamoto zilizojitokeza ni pamoja na watu kusindwa kuingia viwanjani kutokana na kukosa tiketi kwa muda, na wengine kutofahamu namna sahihi ya kununua tiketi hizo kwa njia ya simu za mkononi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Habari wa TFF, changamoto hizo ni za kawaida na zinarekebishika endapo washabiki watafahamu namna sahihi ya kukata tiketi hizo na kwa muda muafaka.

Kwa vyovyote, tiketi hizi ni hatua mojawapo kuelekea uhuru wa mapato ya mlangoni ambako kila shabiki anayeingia uwanjani atafahamika hivyo kuepusha ulanguzi na wizi wa mapato ya mlangoni ambao umekuwa kilio cha wadau kwa kitambo sasa.

Mapya yana mambo yake, kwa muda wa miongo kadhaa washabiki wa hapa nyumbani wamezoea utaratibu wa kununua tiketi mara wafikapo viwanjani. Utaratibu ambao umechochea ulanguzi, kwani walanguzi hununua tiketi nyingi kisha kuwauzia washabiki pale ambapo za halali zinakuwa zimeisha.

Ushirikina

Kama kawaida yetu, shirki imetawala soka letu kama ambavyo soka lote a Afrika limetawaliwa na imani hizi. Katika Uwanja wa Jamhuri, watu wa dawati la ufundi la Yanga walikwenda kutoa glovu za akiba za Kipa wa Mtibwa, kwa kile ambacho kilidhaniwa kuwa ni imani za kishirikina.

Tukio kama hili lilijitokeza tena msimu uliopita katika mchezo wa Simba na Yanga ambapo wachezaji wa Yanga walienda kulitoa taulo la kipa wa Simba, Ivo Mapunda ambalo lilikuwa limetundikwa golini kwake, sababu zikiwa ni zile zile.

Ushirikina si kitu ambacho kinaweza kuwa na madhara ya moja kwa moja katika soka, lakini ni kitu hatari endapo kitaendekezwa. Wachezaji wengi wamekuwa wakilaumu wachezaji wenzao kuwafanyia vitendo vya kishirikina hivyo kuwapunguza ufanisi wao mchezoni.

Pia timu kubwa kabisa zimewahi kuripotiwa kutumia mbinu hizi ili kupata ushindi katika michezo ya ligi kuu kwa kutumia kile ambacho kimekuwa kikifahamika kama ‘Kamati za Ufundi’.

Ni wakati wa timu, wachezaji, na washabiki kutafakari chanzo cha anguko au kufanya vibaya katika mechi kuliko kuegemea imani za kishirikina. .

Matarajio

Ni mapema sana kutoa uelekeo wa Ligi Kuu kwa kuwa ndio kwanza mcezo mmoja umechezwa na kila timu na timu hucheza mechi 26 ili kukamilisha msimu mzima.

Tunaweza kuwa na ligi bora kuliko misimu iliyopita kwani maendeleo katika sekta ya kiufundi miongoni mwa timu za ligi kuu huwa kipimo cha kufanya vizuri.

Kuibuka kwa timu ngeni ambazo zimepania kutoa changamoto I jambo lingine ambalo linaashiria ligi bora msimu huu. Azam, ambao ni mabingwa watetezi wapo katika ubora wao, sawasawa na vilabu vya Simba na Yanga ambavyo vimefanya usajili kabambe.

Uwepo wa Mbeya City, waliosika nafasi ya tat msimu uliopita unaongeza utamu wa ligi yenyewe, n zaidi wanaongezwa nguvu na udhamini wa shilingi 180M kwa mwaka kutoka kampuni ya Binslum Tyres ya Dar es Salaam.

Masuala ya udhamini pia yameongezeka tofauti na misimu yote. Licha ya udhamini wa jumla kutoka kwa mdhamini mkuu, kampuni ya Vodacom, bado kuna mdhamini wa matangazo, ambao ni Azam Media.

Zaidi ya hayo, timu kadhaa zina wadhamini binafsi, ambazo ni Azam (NMB), Yanga (TBL, CRDB), Mbeya City (Binslum), Simba (TBL, Benki ya Posta), Ndanda (Binslum), Coastal Union(Pembe Mill) na Stand United (Binslum).

Kwa muda mrefu fedha kimekuwa kikwazo cha timu kutofanya vema mashindanoni, naamini msimu huu utakuwa na utofauti kwani nusu ya timu zina udhamini wa uhakika.

CREDIT: FIKRA PEVU

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top