Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kata ya
Mbuzii (hawapo pichani).Katibu Mkuu leo alianza ziara yake katika kata
ya Mbuzii ambapo alishiriki ujenzi wa ofisi ya chama sehemu ambayo
inahistoria kwani ilitumika kwa kufanya mikutano ya harakati za kutafuta
Uhuru na ni sehemu iliyojengwa ofisi ya kwanza ya Tanu wilaya ya
Lushoto.
Wananchi wa kata ya Mbuzi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi pamoja na Mbunge
wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba wa ofisi ya CCM kata ya
Mbuzii ,Mbuzii ndio chimbuko la TANU wilaya ya Lushoto.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiendesha bodaboda baada ya Katibu
Mkuu wa CCM kumaliza kufungua shina la madereva bodaboda shina la Dule B
ambapo mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh.January Makamba alitoa pikipiki
moja.
Mkuu wa
Wilaya ya Lushoto Mh. Majid Mganga akiendesha boda boda kuelekea kwenye
uzinduzi wa shina la wajasiriamali la Maisha Plus kata ya Dule.
Baadhi ya mazao yanayolimwa na kikundi cha ujasiriamali Maisha Plus
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba
akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus wakati wa ziara ya Katibu mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
Wakazi
wa kata ya Dule B wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao kabla
ya kuzinduliwa kwa shina la wajasiriamali la Maisha Plus.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha
Plus ambapo alizindua shina la CCM wajasiriamali wa Maisha Plus katika
kata ya Dule B
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupasua mawe kwenye
kambi ya Maisha Plus ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijiandaa kuukata muwa pamoja na
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba
Kazi na Dawa! Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila muwa
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuelekeza Mbunge wa Jimbo la
Bumbuli Mheshimiwa January Makamba namna ya kupiga randa .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya chama baada
ya kuzindua shina la Maisha Plus lililopo Dule B ,jimbo la Bumbuli
wilaya ya Lushoto.
Maisha Plus Bumbuli.
Katibu
Mkuu wa CCM, akiwapungia wananchi mikono alipowasili kwenye mkutano wa
hadhara katika Kata ya Mponde, Jimbo la Bunburi, ambapo aliwahakikishia
wananchi kulitafutia ufumbuzi tatizo la kufungwa kwa kiwanda cha chai
cha Mponde wilayani Lushoto,Mkoani Tanga.
Kinana
aliwataka viongozi wote wa CCM na Serikali waliohusika kufungwa kwa
kiwanda hicho na kuwasababishia adha wananchi kuwajibika wenyewe au
kuwajibishwa.
Umati wa watu ulivyofurika kwenye eneo la mkutano wa hadhara.
Meza kuu wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipokuwa akihutubia wakazi wa Mponde.
Katibu wa
Nec Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mponde ambapo
aliwaambia kuwa CCM ndio chama pekee kinachoweza kumaliza mgogoro wao wa
miaka mingi na sasa ndio wakati umefika wa kulimaliza kabisa.
Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijadili jambo na Mbunge wa Bumbuli
Mh.January Makamba mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mponde.
Kila kona ya uwanja watu walijazana kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya
Mponde ambapo aliwaambia suala lao la matatizo katika kiwanda cha chai
amelichukua na atarudi kwao baada ya mwezi mmoja akiwa na majibu.
Mbunge
wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba akihutubia wananchi wa
Mponde wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana.
Abdulkarim
Jambia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kata ya Vuga akionyesha juu kadi
yake ya CCM baada ya kurejea rasmi CCM kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika Mponde.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijionea namna mashamba ya chai
yalivyogeuka vichaka . Katibu Mkuu ameongozana na Mbunge wa Jimbo la
Bumbuli Mheshimiwa January Makamba.
Post a Comment