Nembo ya Dira ya Jukwaa la Katiba Tanzania.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba
Tanzania (Jukata) Deus Kibamba (kulia), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mambo muhimu ya
kuzingatiwa baada ya makubaliano ya kuahirisha mchakato wa Katiba Mpya
baada ya Uchaguzi Mkuu 2015. Kushoto ni Mratibu wa Mtandao wa Mapambano
ya Ukimwi kwa Wanaume Tanzania (WOFATA), Alex Margery. )
Mwenyekiti wa
Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) Deus Kibamba (kulia), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mambo
muhimu ya kuzingatiwa baada ya makubaliano ya kuahirisha mchakato wa
Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa
Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) Deus Kibamba (wa pili kulia)
akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mratibu wa Jukata, Diana
Kidara, Mratibu wa Mtandao wa Mapambano ya Ukimwi kwa Wanaume Tanzania
(WOFATA), Alex Margery na Mjumbe wa Bodi kutoka Shirikisho la Vyama vya
Watu wenye ulemavu Tanzania (Shivyawata), Maria Chale.
Wapiga picha wa vyombo vya habari wakichukua tukio hilo.
JUKWAA la Katiba Tanzania
(Jukata) limesema iwapo Bunge maalumu la Katiba litaendelea mjini Dodoma
baada ya mchakato wake kusitishwa kupisha uchaguzi mkuu wa 2015
watakwenda kufunga kwa kufuri milango ya jengo hilo ili kuokoa fedha za
watanzania zinazotumika vibaya kwa kulipana posho.
Katika hatua nyingine Jukata
limetangaza jimbo la uchaguzi la Samueli Sita kuwa lipo wazi na nafasi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Fredirick Werema kuwa wazi baada ya
kuwatuhumu kuchangia kwa kiasi kikubwa kuharibu mchakato huo wa katiba
mpya.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba wakati akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mambo muhimu ya
kuzingatiwa baada ya makubaliano ya kuahirisha mchakato wa Katiba Mpya
baada ya Uchaguzi Mkuu 2015
“Nafasi za Sita na Werema
tunatangaza kuwa sasa zipo wazi baada ya kupoteza sifa za kuongoza
kufuatia kuvuruga mchakato wa katiba mpya na kuwa katika kipindi cha
miaka 10 hawatakiwi kugombea nafasi yoyote katika nchi hii hata iwe ya
mjumbe wa shina” alisema Kibamba.
Kibamba alivipongeza vyama vya
siasa vilivyochini ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwa
makubaliano yaliyofanyika na Rais Jakaya Kikwete Agosti 8 mwaka huu
Ikulu ndogo ya Chamwino Dodoma kuwa ni ya faraja na matumaini makubwa
kwa taifa.
Alisema kutokana na mazungumzo
hayo imekubalika kuwa mchakato wa Katiba mpya uahirishwe kwa sasa hadi
baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015.
Akizungumzia kuhusu kufunga
milango ya jengo la Bunge ili asiingie mtu alisema hilo litafanyika
baada wiki mbili kuanzia leo iwapo tu wabunge hao wataendelea na
mchakato wa katiba hiyo na kuwa tukio hilo watalifanya kwa umoja wao.
Kibamba aliongeza kuwa kutokana
na masuala ya Katiba kuwa na unyeti kwa taifa zima na kwa jinsi
yanavyoshikamana na masuala ya uchaguzi ambayo nayo yana wadau wengi nje
ya wanasiasa Jukata wanaona kuna haja ya kupanua wigo wa mazungumzo na
makubaliano yanayoendelea na yatakayokuja siku na miezi ijayo yawe kwa
taifa zima na si kwa wanasiasa.
“Jukata pia tunapongeza uamuzi
wa wanasiasa kuahirisha uchaguzi wa serikali za mitaa uliokuwa ufanyike
mwezi Septemba 2014 mpaka mwaka 2015 hata hivyo zipo hoja za msingi
kuhusu uchaguzi huo” alisema Kibamba.
Post a Comment