Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutumia katika mkutano wa
hadhara mjini Kimanzichana, wilayani Mkuranga, Pwani , alipoanza zira ya
kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi
inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana aliwataka viongozi wa chama na serikali waliojilimbikizia vyeo na kushindwa kutekeleza wajibu wao, waanze kujiuzulu baadhi ya vyeo ili wapatiwe wengine wasio na vyeo kwa lengo la kukiendeleza chama na shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.
01.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na chipukizi
wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Kipala Mpakani, wilayani Mkuranga,
alipoanza ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi
inayotekelezw
02.Kinana akikagua gwaride la chipukizi wakati wa mapokezi hayo.
Nape (kulia) akiwaongoza wananchi kubeba matofali ya kujengea jengo la
maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Adam Malima (kulia)akiwaongoza wananchi
kubeba matofali ya kujengea jengo la maabara katika Shule ya Sekondari
ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao akihutubia katika mkutano wa hadhara na kumkaribisha Katibu Mkuu wa chama hicho, Kinana kuhutubia na kusikiliza kero za za wananchi katika Kijiji cha Kimanzichana.
Kinana akisalimiana na wananchi
Mwendesha bodaboda akiwa amelala baada ya kugongwa na gari wilayani
Mkuranga katika Barabara Kuu ya kutoka Dar kwenda Mtwara. Msafara wa
Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana ulisimama kwa muda katika eneo
hilo na viongozi wa CCM akiwemo Kinana waliteremka kwenye magari na
kusaidia kubeba majeruhi kuwaweka kwenye magari kuwawahisha kwenda
hospitali kwa matibabu.
Baadhi viongozi na wanachama wa CCM waliokuwa kwenye msafara wa Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinanawakisadia kumbeba mwendesha bodaboda
alijeruhiwa baada ya kugongwa na gari wilayani Mkuranga, wakimpeleka
kwenye gari ili awahishwe kwenda hospitali kwa matibabu. Baada ya kufika
kwenye tukio hilo Kinana alisimamisha msafara wake na kwenda kusaidia
majeruhi wa ajali hiyo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kimanzichana.
Kinana akisaidia kujenga jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga.
inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana aliwataka viongozi wa chama na serikali waliojilimbikizia vyeo na kushindwa kutekeleza wajibu wao, waanze kujiuzulu baadhi ya vyeo ili wapatiwe wengine wasio na vyeo kwa lengo la kukiendeleza chama na shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao akihutubia katika mkutano wa hadhara na kumkaribisha Katibu Mkuu wa chama hicho, Kinana kuhutubia na kusikiliza kero za za wananchi katika Kijiji cha Kimanzichana.
Gari lilihusika katika ajali na bodaboda likiwa kichakani baada ya kuacha njia |
Kinana akisaidia kujenga jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga.
Post a Comment