Wajumbe zaidi ya 100 kutoka nchi wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC) wanahudhuria mkutano wa siku mbili wa Jukwaa la
Katibu Mkuu wa EAC kuhusu sekta binafasi na vyama vya kirai mjini Entebe,
Uganda.
Kauli
mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni:''ECA:Nyumbani Kwangu,Biashara Yangu''. Mkutano
wa kwanza wa aina hiyo ulifanyika, Dar es Salaam, Tanzania na wa pili
ulifanyika Nairobi, Kenya.
Naibu
Katibu Mkuu wa EAC,anayeshughulikia Uzalishaji na Sekta ya Jamii, Jessca Eriyo
alisema kwamba lengo la Jukwaa hilo ni kutoa nafasi kwa majadiliano ya moja kwa
moja kati ya Katibu Mkuu wa EAC na Sekta Bnafsi, Vyama vya Kiraia na makundi
mengine juu ya namna ya kuboresha mchakato mzima wa mtangamano wa EAC.
Aliongeza
kwamba : ''Jukwaa litatoa nafasi ya kujadili juu ya fursa na changamoto
zinaopatiakana kutokana na mchakato wa mtangamano na kubadilishina uzoefu.''
Mada
mbalimbali zitawasilishwa katika mkutano huo.
Post a Comment