PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: JAJI MKUU MSTAAFU AGUSTINO RAMADHANI ACHAGULIWA KUWA RAIS WA MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU AFRIKA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  JAJI MKUU  Mstaafu wa Tanzania,Agustino Ramadhani amechaguliwa kuwa rais wa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika(AfCHPR) , kwa ...



 


JAJI MKUU  Mstaafu wa Tanzania,Agustino Ramadhani amechaguliwa kuwa rais wa
Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika(AfCHPR) , kwa kipindi cha
miaka miwili hadi mwaka 2016.
Pia katika jopo la majaji hao Elsie Thomposon kutoka Nijeria naye
ameibuka kidedea kwenye uchaguzi huo uliofanyika juzi katika viwanja vya
mahakama hiyo na kushika nafasi ya kuwa makamu wa Rais wa mahakama
hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya uchaguzi huo kuisha,
Jaji Mstaafu Ramadhani alishukuru kwa majaji wenzake kumchagua
kuiongoza mahakama hiyo kwa kipindi hicho.
Aidha alisema kuwa katika nafasi aliyoipata ni sifa kubwa kwa nchi ya Tanzania na nchi
za Afrika kwani kwa Tanzania nafasi hiyo ni changamoto ya
kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na kuheshimiwa na kila mtu.
“Nawashukuru wenzangu kwakuniichagua na pia hii ni sifa kwa nchi yangu
na wenzetu wakiona tunafaa kuongoza tunaweza tena mara baada ya
kumaliza nafasi zetu mwaka 2016 , hivyo hii ni heshima kwa Taifa
letu”.
Jaji Ramadhani amepata nafasi hiyo mara baada ya aliyekuwa Rais wa
mahakama hiyo, Jaji Sophia na Akkufo kumaliza muda wake.
Awali kulitanguliwa na kuwaapisha majaji wengine wapya watatu ambao ni
Jaji Rafaa Achour kutoka Jaji Solomy Basa , pamoja na Jaji Angelo
Mahesa ambao wameapishwa jana kuziba nafasi zilizoachwa wazi na
majaji wengine watatu waliomaliza muda wao akiwemo Akuffo .
Halfya ya kuapishwa kwa majaji hao pia ilihudhuriwa na viongozi wa
dini kutoka mahehebu mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali.
Mara baada ya kuapishwa kwa majaji hao na uchaguzi kumalizika Rais
wa mahakama hiyo, Jaji mstaafu Ramadhani alisema kuwa kazi ya
mahakama hiyo ni kusimamia haki za binadamu pamoja na kuhakikisha
inatoa maamuzi katika kesi mbalimbali zilizofikishwa mahakamani hapo .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top