PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HALI YA HEWA WATABIRI MVUA KUBWA KUNYESHA MWEZI WA SEPTEMBER
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
   MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetahadharisha kuwa mvua zinazotarajiwa kuanza mwezi Septemba hadi Disemba mwaka huu zitakua...
  


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetahadharisha kuwa mvua zinazotarajiwa kuanza mwezi Septemba hadi Disemba mwaka huu zitakua kubwa katika baadhi ya maeneo na hivyo kuweza kuambatana na madhara ikiwemo mafuriko na magonjwa ya milipuko.

Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agness Kijazi, kwa waandishi wa habari mjini Morogoro Alhamisi Septemba 4, 2014, imebainisha kuwa mvua hizo zinatokana na ongezeko la joto la baharini katika kipindi mwanzoni mwa Juni hadi Agosti 2014.

Alisema joto la uso wa bahari (SST) mashariki mwa bahari ya Pasifiki na kusini-magharibi mwa bahari ya Hindi liliongezeka huku joto la bahari ya Atlantiki mashariki na kaskazini- mashariki likiwa la wastani.
 Amesema, msimu wa mvua za vuli zinazotarajiwa kunyesha zinatarajiwa kuwa kubwa (wastani hadi za juu ya wastani) katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini (mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Hali hiyo pia itaihusu maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, na Manyara) pamoja na mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Amebainisha ya kuwa mvua hizo zinataraijwa kuanza wiki za kwanza ya Septemba, Octoba na Novemba na kuwa katika maeneo ya Ukanda wa Pwani (mkoa wa Tanga na Kisiwa cha Pemba) na katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki.

Akizungumzia athari ya msimu uliopita amesema maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka ya Nyanda ya Juu Kusini Magharibi (Vituo vya Mbeya, Tukuyu, Mahenge, vilipima mvua za juu ya wastani na Kituo cha Sumbawanga kiwango cha mvua kilikuwa cha wastani), Kanda ya Magharibi (mkoa wa Kigoma, Kibondo na Tabora vilionyesha mvua za wasatani), Pwani ya Kaskazini (Vituo vya Mtwara vilionyesha mvua za wastani).

Pia amesema maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka ikiwemo Kanda ya Ziwa Victoria vipimo vya Bukoba na Musoma viliwa vya wastani na katika Kituo cha Shinyanga kilipima mvua kiwango cha wastani wakati katika kituo cha Mwanza kiwango cha mvua kilikuwa chini ya wastani.

“Nyanda za Kaskazini Mashariki katika Vituo vya Arusha, Lyamungo na Kilimanajaro vilionyesha kuwa mvua za wastani, ilihali vituo vya Moshi, Same kiwango cha mvua kilikuwa cha wastani na kuwa Pwani ya Kaskazini na Visiwa vya Unguja na Pemba ilionyesha kuwa vituo vya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pemba vilipima mvua za juu ya wastani na vituo vya Zanzibar, Amani, Kizimbani, pamoja na Tanga mvua zilikuwa za wastani”.

Amesema maeneo ya Magharibi mwa nchi, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini-Magharibi, Kusini mwa nchi na Pwani ya Kusini katika kipindi cha Octoba hadi Disemba 2014 yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Mamlaka imetahadharisha kuwa mamlaka zinazohusika na maafa kuchukua hatua stahiki katika utunzaji wa mazingira, upatikanaji wa maji safi na salama na usambazaji wa madawa, maji na chakula ikiw ani pamoja na hatua za kujiandaa na kukabiliana na majanga yanayoweza kitokea kutokana na vipindi vya mvua.

Imeelezwa kuwa mamlaka nyingine kama Mali asili na Utalii, Maji na Nishati, Mamlaka za Maji, Sekta za Afya, malisho ya maji kwa kifugo na wanyamapori kuchukua tahadhari zinazoweza kutokea ili kutunza miundombinu kama ya barabara za maeneo husika dhidi ya athari za mvua kubwa za za juu ya wastani katika maeneo husika.f

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top