BENKI YA DUNIA YAAINISHA SEKTA ZENYE TIJA KWENYE AJIRA TANZANIA
RIPOTI ya hivi karibuni iliyotolewa na Benki ya Dunia imeainisha kuwa kilimo cha mazao yenye thamani kubwa ikiwemo maua, viungo, utalii na sekta ya viwanda vya ngozi ni maeneo yanayoweza kuongeza ajira zenye tija kwa wananchi wengi kutoka mashambani ili kupunguza umasikini utakaokuza ustawi wenye uwiano sawa na kwamba hiyo ni moja ya sababu itakayoondoa tatizo la ajira nchini katika siku za mbeleni.
Inaelezwa kuwa, sababu inayoweza kukuza uchumi wa Tanzania ni kuangalia nyanja tatu za viwango vya juu vya umaskini, ongezeko la watu na kundi la watu wanaohama kutoka vijijini kwenda mijini, pia katika mapendekezo ya mpango huu mambo (12) muhimu yaliyopangwa kwenye misingi mitatu ili kuongeza kazi zenye tija nchini Tanzania.
Hayo yapo kwenye uzinduzi wa ripoti ya ‘Ajira Zenye Tija’ uliofanywa baina ya Benki ya Dunia, World Bank (WB) na Tume ya Mipango, ripoti hiyo imependekeza kuboresha kilimo ili kusaidia wawekezaji wadogo na kuanzisha uzalishaji wa huduma na bidhaa viwandani ili mpango huu uweze kwenye sekta nyingi ikiwemo kuzalisha ajira zenye tija
Hata hivyo, imeeleza kuwa njia tatu zinazoweza kutumika kuzalisha ajira zenye tija nchini ni pamoja na kukuza biashara ndogo ndogo zisizotokana na kilimo, ambazo zimekuwa zikikua kwa haraka wakati wa kupanuka kwa haraka kwa miji. Nguzo hizo zinaweka msisitizo kwenye mashamba kutokana na naeneo hayo kuwa yenye sehemu kubwa ya ajira nchini, wakati nguzo pia moja ya nguzo huzo ikijadili uwezo wa kujenga ajira kunakohusiana na kupanuka kwa biashara na kuingia kwenye masoko mapya.
Imeeleza kuwa vipo vikwazo kwenye masoko kwa namna ya upatikanaji finyu wa mikopo, ukosefu wa umeme wa uhakika, ujuzi mdogo wa watu walio wengi na kuachana na kilimo duni na kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji wa bidhaa na huduma ili kuendeleza biashara ndogo ndogo ili ujasiriamali uzalishe ajira bora kwa wananchi wengi.
Ripoti hiyo pia imependekeza kuwa katika sekta ya kilimo kibadilike kutoka hali duni iliyopo sasa kwa kutumia pembejeo na teknolojia ya kisasa, ili kuweza kuongeza thamani na kuuza bidhaa zake kwenye masoko ya kikanda nan je ya nchi.
“Mpango kazi uliopendekezwa unatambua hatua kuu 12 zilizoandaliwa zikizingatia nguzo kuu tatu zilizoainishwa hapo juu zitasaidia ili kukuza utengenezaji wa kazi zenye tija hapa nchini Tanzania,kwa wengi, idadi hii inaweza kuonekana kuwa kubwa sana (hasa ukichukulia kwamba hatua hizi zimegawanywa tena katika hatua nyingine zaidi, kipengele kwa kipengele)”.
Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha kuwa changamoto ya ajira zenye tija haiwezi kukidhiwa kiuhalisia kwa hatua chache za juu juu, ni suala ambalo kiasili ni mtambuka na ukubwa wa mageuzi yanayohitajika kuhimiza kujenga kazi zenye tija kunahitaji matumizi na utekelezaji wa mpango kazi jumuishi.
Shabaha ya utafiti huu imebainishwa kuwa ni kuchangia katika mjadala kuhusu kujenga ajira nchini Tanzania kwa kupendekeza mwelekeo katika kutunga sera, kwani sekta ndogo zimebainika kuwa ndizo zilizobainishwa kwenye utafiti huu na kwamba zipewe kipaumbelena kwamba hatua mahususi zipendekezwe ili kuimarisha msingi wa kiuchumi na mazingira shindanishi ambayo ni muhimu kwa biashara kushamiri na kutengeneza kazi zenye tija, uzoefu katika utendaji wa kimataifa utumika pale inapowezekana ingawa hatua hizi zilizopendekezwa haziwezi kushughulikia vikwazo vyote vinavyoyakabili makampuni nchini Tanzania, bali zinatoa mwelekeo wa vipaumbele vinavyohitajika zaidi.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa ripoti hiyo, alisema serikali imefanya jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa kazi zenye tija kwa kufanya utafiti wa vikwazo vya uwekezaji uliofanywa na Taasisi ya Rais ya Matokeo Makubwa Sasa (MMS) na kubainisha changamoto za ukosefu wa taaluma, mzigo wa kodi, urasimu, rushwa, na ardhi kwa wawekezaji.
“Kwa sasa Tanzania wafanyakazi wenye uwezo wa kufanyakazi wanakadiriwa kufikia milioni 20 lakini kati ya hao milioni 19 wameajiriwa katika sekta zilizo rasmi na zisizo rasmi” alisema.
Akizungumzia ripoti hiyo, Rais Kikwete, alisema imeibua changamoto nyingi za ukosefu wa ajira na namna zinavyoweza kuondolewa.
Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Jacques Morisset, anasema utatuzi wa ukosefu wa ajira ni suala linalohitaji kutekelezwa kwa mapana yake huku akisema njia zinazoweza kutumika kuzalisha ajira zenye tija nchini ni kukuza biashara ndogo ni kuachana na kilimo duni na kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji wa bidhaa na huduma.
Tanzania inahitaji kuandaa ajira zenye staha kwa watu wasio na ajira wanakadiriwa kufikia milioni 40 ifikapo mwaka 2030
Post a Comment