PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WATU SABA WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ZA DOLA ZA KIMAREKANI JIJINI DAR ES SALAAM
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam akionesha fedha bandia zilizokamatwa Jeshi la Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es...


Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam akionesha fedha bandia zilizokamatwa

Jeshi la Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za dola ya Kimarekani huko maeneo ya Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na dola 1,064,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni moja katika

nyumba namba 07 walimokuwa wamepanga.

Polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kuweka mtego ambapo askari walifika katika eneo hilo na kuwatia mbaroni watuhumiwa wakiwa na noti hizo bandia zilizokuwa zimefungwa mabunda themanini na kasiki ndogo ambayo imefungwa kwa namba za siri.

Aidha watuhumiwa walikiri kujihusisha na utengenezaji wa noti bandia.

Watuhumiwa hao ni:-
1.AHMAD S/O MOHAMED Miaka 50, mfanyabiashara, mkazi wa Mombasa Kenya

2.RICHARD S/O MAGOTI Miaka 61, mfanyabiashara, mkazi wa Musoma mkoani Mara.
3.SIMONI S/O LUKIKO Miaka 58, mkazi wa Magomeni Kagera
4.HUMPHREY S/O LEONARD Miaka 34, mlinzi, mkazi wa Mburahati
5.FRANK S/O CHARLES Miaka 31 mfanyabiashara, mkazi wa Sinza
6.ABDALLAH S/O YUSUPH, Miaka 34, mfanyabiashara, Mkazi wa Sinza
7.BAKARI S/O BAKARI, Miaka 31, mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi, Kimara.

Aidha watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top