Walioshuhudia
tukio hilo walisema mwanamme huyo ambaye siyo mwenyeji wa mtaa huo
alikutwa akimchezea sehemu za siri mtoto huyo kisha kuanza kumvutia eneo
la chooni.
“Alimwita
mtoto huyo,akaanza kumchezea sehemu za siri lakini mtoto alipiga
kelele na baada ya kusikia kelele za mtoto huyo tukatoka nje kumsaidi,
tukapiga mayowe kuomba msaada,watu wakajaa wakaja pia viongozi wakiwemo
wa sungusungu wakaanza kumhoji”,alieleza mmoja wa mashuhuda hao ambaye
hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
“Hata
hivyo mtuhumiwa huyo katika hali ya kubabaika alianza kukimbia na
alipoulizwa anatoka wapi hakueleweka mara aseme anatoka Majengo,mara
Nguzo nane,mara Buhangija ndipo wananchi wakaanza kumpiga”,alieleza
shuhuda huyo.
Akizungumzia
tukio hilo bibi wa mtoto aliyenusurika kubakwa bi Marieta Mkaima
ambaye hakuwepo wakati tukio hilo alieleza kusikitishwa na kitendo
hicho huku akiitaka jamii kuendelea kushirikiana katika kulinda watoto
dhidi ya watu wabaya.
“Naishi
na mjukuu wangu,sikuwepo nyumbani nimepigiwa simu kuwa kuna tukio
nyumbani,ndiyo nimekuta umati wa watu,mwanamme alitaka kubaka mjukuu
wangu”,alieleza bibi wa mtoto huyo.
Kamanda
wa sungusungu mtaa wa Mwamala Anthony Shija aliiambia malunde1 blog
alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mwanamme huyo alikuwa amebeba mtoto na
kuanza kumshika shika sehemu za siri lakini mtoto katika kujihami kwake
mtoto alifanikiwa kumponyoka mikononi mwa mtuhumiwa huku akipiga
kelele.
“Baada
ya mtoto kuondoka mikononi mwa mtuhumiwa jamaa alimvuta tena ili
akidhi haja zake,mtoto akaendelea kupiga kelele ndipo majirani
wakajitokeza kumsaidia na kutokana na wananchi kuchoshwa na matukio ya
ukatili dhidi ya watoto ndiyo maana wakajitokeza kwa wingi”,alieleza
kamanda wa sungusungu.
“Tumepiga
simu polisi,tumekuta anapigwa na wananchi,sisi viongozi tumejitahidi
kuzuia mtuhumiwa asiuawe kwani wananchi wana hasira sana,wengine
wamebeba mawe,fimbo na virungu”,alifafanua kamanda wa sungusungu.
Naye
diwani wa viti maalum kutoka kata ya Masekelo bi Zainabu Kheri
alilaani kitendo kilichofanywa na mwanamme huyo huku akiitaka jamii
kuimarisha ulinzi kwa watoto bila kujali ni wako au la kwani vitendo
vya ukatili dhidi ya watoto hivi sasa ni tishio katika manispaa ya
Shinyanga.
“Nikiwa
kama mzazi nawaomba wazazi wenzangu na jamii kwa ujumla kulinda
watoto,pia wanaofanya vitendo hivi waache tabia hizo na wamwogope mungu
pia,kwani ni laana kubwa kubaka,kulawiti na kutoboa macho watoto
wasiokuwa na hatia”,alieleza diwani huyo.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wanamshikilia
mtuhumiwa na uchunguzi unaendelea.
“Tulipata
taarifa kuhusu wananchi kujichukulia sheria mkononi,tukaenda kumwokoa
mtuhumiwa,sasa tunamshikilia,na uchunguzi zaidi unaendelea”,alieleza
kamanda Kamugisha.
Tukio
la mtoto kunusurika kubakwa limekuja ikiwa ni siku chache tu baada ya
mtoto Hapiness Kashinje aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika shule
ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga kuuawa
kwa kubakwa kisha kutobolewa macho Agosti 25 mwaka huu katika kitongoji
cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi manispaa ya
Shinyanga.
Post a Comment