Home
»
»Unlabelled
» TIBA NA KINGA YA UKIMWI YAGUNDULIWA HUKO MAREKANI
Watafiti wakitoa sampuli za damu kutoka kwa sokwe mtu katika utafiti wa Ukimwi huko Gabon.
Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa.
Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia
waandishi wa habari juzi mjini Philadelphia, Marekani kuwa tofauti na
utafiti mwingine, wao wamegundua namna ya kukiondoa kirusi kilichoingia kwenye kinasaba (DNA) ndani ya CD4 na kukitoa nje na hatimaye kukiua.
Alisema dawa hiyo inafanya kazi hiyo bila kuathiri seli za mwili wa binadamu.
Dk Khalili alisema
ugunduzi wao ni wa hali ya juu zaidi kwa sababu teknolojia ya
kutengeneza dawa hiyo ni tofauti na nyingine zilizokwisha kugunduliwa
ambazo hazina uwezo wa kupenya ndani ya seli za binadamu, bali kuathiri
tu VVU vilivyopo nje yake, ndani ya mfumo wa damu.
“Dawa yetu inakivuta kirusi nje ya seli (CD4) bila
kuiathiri seli yenyewe na kukiua. Hivyo dawa hii itatumika kwa muda
fulani na kuua virusi vyote mwilini na hakuna haja ya kuitumia wakati
wote kama ilivyo dawa ya kufubaza VVU (ARV).”
ARV huangamiza VVU vilivyopo kwenye damu na
kuendelea kuviacha hai vile ambavyo tayari vimeingia ndani ya CD4, hivyo
kufanya virusi kuzuka upya pindi mwathirika anapoacha kutumia dawa.
Mmoja wa wataalamu katika Taasisi ya Taifa ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kituo cha Mbeya (NIMR-MMRC), Clifford
Majani ameuelezea utafiti huo kama mwanga mpya katika teknolojia ya
kukabili VVU.
“Kama imepatikana teknolojia ya kukiondoa kirusi
ndani ya seli ni hatua nzuri ya kukabili VVU. Hili lilionekana kuwa gumu
mwanzoni,” alisema Majani.
Alisema imekuwa vigumu kuua kirusi kikiwa ndani ya
seli na hata baadhi ya wanasayansi wamejaribu kutengeneza dawa
itakayotambua seli zilizoathirika ili ziuawe lakini hilo likawa gumu.
“Inaweza ikapatikana dawa ya namna hiyo (inayoua
seli zilizoathirika) lakini ikawa inaathiri vitu vingine ndani ya mwili.
Hilo halikubaliki. Kikubwa katika ugunduzi huo ni dawa kuweza kukifuata
kirusi kinakojificha na kukiondoa, jambo ambalo dawa nyingi zimeshindwa
zikiwamo ARV,” alisema.
Hata hivyo, Majani alisema changamoto ambayo inaweza kujitokeza katika majaribio ya dawa hiyo ni usalama wakati wa matumizi.
About Author

Advertisement

Recent Posts
- The Maasai Families in Longido District allegedly use baptism ceremonies to conceal FGM practices17 Sep 20240
By our Reporter in Longido Some Maasai families in Longido District, Arusha Region ar...Read more »
- Tanzanian Shillings 6.56 Trillion Investment in the JNHPP Project Bears Fruits for the Nation14 Sep 20240
By Our ReporterThe Public Investments Committee (PIC) of Parliament visited the construction site of...Read more »
- 35 teams set to battle in Chem Chem Cup 2024: Sh78 million up for grabs10 Sep 20240
By Mussa Juma, MaipacBabati. A total of 35 teams will participate in the 2024 Chem Chem Cup, costin...Read more »
- Mwiba holdings Donates house for Health Workers and 194 bicycles to Meatu students.29 Aug 20240
By Our Staff Writer in MeatuMwiba Holdings Ltd, a tourism and conservation investment company ...Read more »
- Mount Kilimanjaro porters' jobs in jeopardy due to foreign influence and controversial practices29 Aug 20240
KPAP's influence has shifted the tourism market, with foreign agents favoring their affiliates over ...Read more »
- Tanzania ramps up health education amid Mpox threat25 Aug 20240
By Staff WriterIn a bold move to safeguard Tanzania from the looming threat of Mpox, the Ministry o...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.