MATUMIZI YA VIPODOZI, VIROBA NI JANGA LA KITAIFA A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: MATUMIZI YA VIPODOZI, VIROBA NI JANGA LA KITAIFA Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: SERIKALI imetakiwa kutangaza tatizo la matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya sumu na pombe haramu za viroba kuwa janga la Taifa, ka... SERIKALI imetakiwa kutangaza tatizo la matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya sumu na pombe haramu za viroba kuwa janga la Taifa, kama ilivyo kwa dawa za kulevya nchini, kutokana na uingizwaji wa bidhaa hizo mkoani Mbeya kukithiri kwa kiwango kikubwa na kuathiri afya za watumiaji na kusababisha wengine kufariki kutokana na kutumia bidhaa feki. PRINCEMEDIA TZ imejulishwa kuwa tatizo la kushamiri kwa bidhaa hizo katika mkoa wa huo umeongezeka mara dufu, licha ya serikali kupiga vita uuzwaji wa bidhaa feki ikiwemo vipodozi na pombe haramu ya viroba ambazo huingiwa nchini kinyemela katika mikoa iliyopo pembezoni mwa nchi jirani zinazozunguka mikoa hiyo nchini. Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wametoa kauli hiyo, wakati wakishiriki zoezi la kuteketeza vipodozi vyenye viambata vya sumu na pombe haramu za viroba ambalo limefanywa na Mamlaka ya Chakulana Dawa, Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA) Nyanda za Juu Kusini katika wilaya hiyo. Wananchi hao wamesema pombe hizo zimesababisha vijana wengi wilayani humo kupoteza maisha pamoja na kuathiriwa na vipodozi vyenye sumu vikiathiri vibaya ngozi za watumiaji na kulazimika kutoa kilio hicho kwa serikali ili iweze kutangaza bidhaa hizo kuwa janga la kitaifa ili kunusuru afya za watumiaji. Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka hiyo kutoka Nyanda za Juu Kusini, Yusto Walace, amesema mamlka hiyo imeteketeza bidhaa mbalimbali zilizoingizwa nchini kinyume cha sheria na kuwa (TFDA) itaendelea kupambana na tataizo hilo ili kunusuru afya za watumiaji na kusema kuwa tatizo la kuzagaa kwa bidhaa hizo katika mkoa huo linaathiriwa na uwepo wa njia za panja ambazo hutumiwa na watu wasio waadilifu. Mkuu wa wilaya ya hiyo, Gulam Kifu, pamoja na kukiri kuwepo kwa bidhaa hizo kwa wingi wilayani Mbarali, ameitaka (TFDA) kushirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuongeza kasi ya mapambano dhida ya uingizwaji wa bidhaa hizo na kusema kilio cha vijana hao kutaka kutangazwa kwa janga hilo atakifikisha katika mamlaka husika. Naye, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, amesema kuwa jeshi lake lipo makini kwa kuwakamata watu wote wanaokutwa na dawa hizo pamoja na wale wanaohisiwa kushiriki kuingiza dawa hizo na kwamba wapo watu wamekamatwa kwa muda mfupi na polisi kisha kufunguliwa mashtaka mahakamani. Kilio cha wananchi Baadhi ya wananchi mkoani humo wamesema kushamiri kwa tatizo hilo ni janga kwao na hivyo wameiomba jamii kuhamasishana na kushirikiana na mamlaka hiyo pamoja na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa juu ya watu wanaouza dawa bandia, na kwamba kufanya hivyo itasaidia maradufu kudhibiti uingizwaji na usambazwaji wa dawa hizo zenye hatari katika afya ya binadamu ambazo huwaathiri wananchi kwa kiwango kikubwa. Tafiti zinaonyesha kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikilalamikiwa mara kadhaa kutokana na kushindwa kuwabana wanaoingiza na kusambaza bidhaa hizo kinyume cha sheria katika maeneo tofauti hapa nchini kwa kile kilichotafsiriwa kuwa mamlaka hiyo inawafahamu wanaoingiza bidhaa hizo
Post a Comment