Mabingwa
katika mpira wa miguu na mpira wa Pete(Netball)Chuo cha Arusha
Journalism Training College(AJTC)wakishangilia ushindi wao.
Arusha.Timu ya soka na ya mpira wa pete za Chuo Cha
Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika bonanza la
tisa la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini.
Katika bonanza hilo, lilifanyika katika uwanja wa Sheikh
Amri Abeid kwa kuandaliwa na Taswa Arusha na kampuni ya Ms Unique, jumla
ya timu 10 zilishiriki kutoka mkoa wa Arusha na Manyara.
Timu ya soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa
mikwaju ya penati 5-4 timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu
hiyo, waliwashinda timu ya chuo cha uandishi wa habari na maendeleo ya
jamii (IMS), magoli 18-5.
Mgeni rasmi katika bonanza Mwenyekiti wa Taswa Taifa, Juma
Pinto alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa very soka
alipewa kikombe, ,fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.
Huku mshindi wa pili soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa
mpira wa pete alizawadiwa kikombe cha fedha taslimu 100, 000 huku
mshindi wa pili akikabidhiwa tsh 50, 000.
Katika bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia
nchini, (Tbl), kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi
Ngorongoro, Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na
Alphatel timu nyingine zilizoshiriki ni Radio 5.
Nyingine ni timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa Manyara,
Salam Club, IMS na Taswa Arusha Arusha ambayo iliambulia ushindi
katika kukamata kuku.
Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi the nzuri waliofanya.
Pinto pia aliahidi katika maadhimidho ya miaka 10 ya
bonanza hilo, mkutano mkuu wa T aswa Taifa utafanyik a Arusha sambamba
na tuzo za waandishi bora.
Awali Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi Tbl
kuendelea kudhamini bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na
wakazi wengi wa Arusha.
Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza
wanahabari kwa kushiriki kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kue
kudhamini.
Post a Comment