PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Moto wateketeza soko mitumba la Karume, Manispaa yalaumiwa kuwafanyia hujuma machinga
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  SOKO la Mitumba la Karume lililopo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha...

 


SOKO la Mitumba la Karume lililopo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar
es Salaam, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha
hasara ya mamilioni ya fedha na kuharibu miundombinu ya soko hilo.

Wakizungumza na Kituo hiki Juni 12, 2014 baadhi ya wafanyabiashara
katika soko hilo wamesema mali zote zikiwemo nguo, viatu, mabegi na
bidhaa nyingine, zimeteketea kwa moto na kwa sasa hawaelewi cha
kufanya.

Wamesema kuwa inawezekana chanzo cha moto huo ni hujuma kutokana na
mgogoro ya muda mrefu baina yao na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,
huku wakisema kuwa mgogoro huo umesababishwa na uamuzi wa halmashauri
hiyo kutaka kuwaondoa kwa nguvu kwa madai ya kulifanyia ukarabati soko
hilo bila kuwapatia eneo jingine.

Hayta hivyo, Meya wa Manispaa hiyo, Jerry Silaa, amewataka
wafanyabiashara hao kujiepusha kuwa watabiri na kwamba Halmashauri
inafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

PRINCEMEDIA TZ imeshuhudia tukio hilo na kusababisha kuharibika kwa
miundombinu ya soko hilo, nguzo za umeme, na vibanda mbalimbali vya
wafanyabiashara hao ambapo Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji kilifanya
juhudi za kuzima moto huo kwa muda mfupi, ambapo uliweza kufika karibu
na kiwanda cha kutengeneza bia cha Breweries, huku ukiwa
haujasababisha hasara yeyote katika nyumba za jirani na soko hilo.

Katika tukio hilo hakuna kibada cha biashara kilichosalimika na hakuna
mtu aliyefanikiwa kuokoa mali yayote kutokana na moto huo kuwa mkubwa
na waokoaji kushindwa kuchukua bidhaa zilizokuwepo ndani kutokana na
moto huo kushika kasi kwa haraka.

Hata hivyo, chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni sehemu yenye banda
la kuuzia chakula ‘Mama Ntilie’ ambao inasemekana huchemsha maharage
na kuyaacha usiku ili yaive vizuri na kupelekea moto huo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, amesema 
kuwa tukio hilo lilitokea Jumatano Juni 11, 2014 saa 9:15
usiku na kusema moto huo ulianza kuwaka katikati ya soko hilo na
baadae kushika kasi katika maeneo mengine.

Mbali na haayo amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kikosi cha
Zima Moto na uokoaji wanakutana na viongozi wa wafanyabiashara hao ili
kutathmini hasara iliyotokea, huku akisema bado Jeshi hilo linaendelea
na upelelezi wa tukio hilo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top