JUMLA ya watu 35,000 wakiwepo watoto wadogo zaidi ya 3500, wanatumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI,(ARVs) katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative,(AGPAHI's) ambalo linajihusisha na mapambano dhidi ya ukimwi, Laurean Bwanakunu alisema watu hao, wamebainika kuishi na VVU kutokana na kupimwa katika vituo mbali mbali vya afya na hospitali katika mikoa hiyo.
Bwanakunu alisema, shirika lao ambalo limekuwa likijihusisha na tiba na matunzo kwa watu, waliobainika kuambukizwa VVU, katika mwaka fedha 2013/14 limepanga kutumia zaidi ya Tsh 7 bilioni katika mikoa hiyo, katika vita dhidi ya UKIMWI.
Mkurugenzi huyo, alisema shirika hilo, limekuwa na miradi ya kuzuia maambuki ya UKIMWI kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa watoto.
"tafiti zinaonesha kuwa kuna uwezekano wa asilimia 95 wa kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kama mama mjamzito, akipimwa mapema na kuanza kupewa dawa"alisema
Hata hivyo, alisema licha ya shirika hilo, kuwa ma miradi katika mikoa hiyo, bado akina mama wengi wajawazito, wajafikiwa kutokana na idadi yao kuwa kubwa na kuchelewa kupimwa.
"katika mikoa hii bado kuna mila na desturi ambazo zinachangia maambuki ya VVU hivyo juhudi zinahitajika ili kusaidia kuzuia maambukizi mapya na pia kuwatunza walioathirika"alisema.
Awali akitoa mada katika mkutano wa pamoja wa wafanyakazi wa shirika hilo,Dk Amso Nshela alisema katika mikoa hiyo, mitatu shirika hilo, limefanikiwa sana kupunguza maambuki za UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Post a Comment