Meneja Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza enzi za uhai wake.
Na Haruni Sanchawa
JAMBO
limezua jambo! Maswali matano ya msingi yameibuka kufuatia kifo cha
aliyekuwa Meneja Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati
na Maji (Ewura), Julius Gashaza kilichotokea hotelini katika mazingira
ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar akitoka Dodoma
ambako alihojiwa na Kamati ya Bunge ya Bajeti, Amani limeyanasa.
Habari za
kiintelijensia zilidai kwamba marehemu Gashaza ndiye aliyekuwa na
majukumu ya kupanga bei za mafuta kila mwezi, alikuwa mjini Dodoma kwa
siku mbili, Ijumaa na Jumamosi iliyopita kuhusu kuweka wazi kiwango cha
mafuta kinachoingizwa nchini, mgawo wa fedha unaotolewa na Ewura kwenda
kuhudumia umeme katika vijiji (Rea) na fedha za mfuko wa barabara.
Jumapili
iliyopita, meneja huyo alikutwa amekufa kwenye Hoteli ya Mwanga Lodge
iliyopo Yombo-Vituka, wilayani Temeke jijini Dar na kusadikiwa kuwa
alijinyonga kwa tai kwenye nondo za dirisha la chooni katika chumba Na.
113.Mwandishi wetu alifuatilia kwa karibu tukio hilo la kusikitisha na
kubaini mambo kadha wa kadha.
NYUMBANI KWA MAREHEMU
Jumatatu
iliyopita mwandishi wetu alianza kwa kufika nyumbani kwa marahemu lakini
hakuna aliyekuwa tayari kutoa ushirikiano mwa mwanahabari wetu.
Baada ya hapo, mwandishi wetu alikwenda kwenye hoteli hiyo ambako ndiko alikopata maswali hayo matano yenye kuumiza kichwa.
Mhudumu mmoja wa hoteli hiyo ambaye aliomba hifadhi ya jina, alisimulia mazingira yote ya kifo cha meneja huyo, alisema:
“Usiku wa
kuamkia siku ya tukio, marehemu alikuja hapa hotelini akiwa ameongozana
na watu wanne. Wanawake wawili na wanaume wawili akiwemo yeye marehemu.
“Nilisikia
wale wanawake mmoja alikuwa mke wa marehemu, mwingine mke wa rafiki wa
marehemu. Wakachukua chumba, wakaingia ndani wote.
“Baada ya muda, walitoka watatu. Mke wa marehemu, rafiki yake na mke wa rafiki yake.
“Kwa hiyo inamaanisha ndani ya chumba alibaki marehemu, maana si waliingia wanne na wametoka watatu!
“Tulilala!
Asubuhi alikuja yule rafiki wa marehemu akasema anaomba kusaidiwa
kumwona marehemu maana amekwenda kugonga lakini hajaamka na mlango
umefungwa.
“Tulikwenda wote, kufika kweli mlango ulifungwa. Ikabidi tuchukue funguo nyingine kufungua.
“Hakuwemo chumbani na kwenye kitanda palionesha alama ya mtu kukaa tu si kulala kwani palitengeneza duara alipokaa.
“Kwenda chooni ndipo tukamkuta amekufa kwa kujinyonga kwa tai.”
Alisema kwamba ndipo taratibu za kuwaita polisi zilifuata.
MANENOMANENO YA WATU
Kufuatia
hali hiyo, kumeibuka maneno mengi. Wengine wanadai marehemu alinyongwa
na wabaya wake, wapo wanaosema alijinyonga kufuatia uchungu wa kutishiwa
maisha na wabaya wake kuhusu kazi.
Wengine wakaenda mbele zaidi kwa kudai kuwa wanyongaji hao walimfuatilia kwa muda mrefu siku ya tukio.
MASWALI MATANO
Swali la
kwanza: Kama kweli marehemu alinyongwa ni kwa nini mlango ulikutwa
umefungwa kwa ndani? Je, mnyongaji alitokaje baada ya kutekeleza mauaji
hayo?
Swali la
pili: Kama kweli marehemu alinyongwa, kwa nini kitandani kulikutwa na
alama ya mtu kukaa tu na kusiwepo kwa dalili za mapambano au
purukushani?
Swali na
tatu: Kama kweli alijinyonga mwenyewe ni kwa nini iwe kipindi hiki
ambacho inadaiwa alipokea vitisho kutoka kwa wabaya wake kwamba atauawa?
Swali la
nne: Uamuzi wa kuchukua chumba kwenye hoteli hiyo ulitoka kwa nani?
Marehemu mwenyewe au? Kama alishauriwa, aliyemshauri ana cha kujibu?
Swali la
tano: Kama kulikuwa na matatizo ya kikazi kama ilivyodaiwa, basi
Mkurugenzi Mstaafu wa Ewura, Haruna Masebu atakuwa anayajua hivyo
angeweza kusaidia kuyasema.
Swali
lingine ambalo lingeweza kuongeza idadi ni juu ya uwezekano wa kuingizwa
kwa funguo nje wakati ya ndani ilizungushwa lakini imebainika kwamba
baada ya funguo kufungwa na mlango kuwa ‘lokdi’, funguo hiyo huwa ‘luzi’
tena hivyo mwenye funguo nje anaweza kuisukuma na kuingiza nyingine.
ALIWAHI KUSIAIDIA GLOBAL KUPATA KIBALI CHA KAMPUNI YA KUINGIZA MAFUTA
Marehemu
atakumbukwa na uongozi wa Kampuni ya Global Publishers kwani aliwahi
kuisaidia kupata kibali cha kuingiza mafuta nchini bila mizengwe wala
kutaka shukrani.
Kwa
mujibu wa Meneja wa Masoko wa Global Publishers na Kampuni ya Shigongo
Oil, Benjamin Mwanambuu, marehemu alikuwa akifanya kazi yake kwa kufuata
utaratibu na sheria.
“Kwa
kweli nilimfahamu marehumu Gashaza wakati wa kutafuta kibali cha
kungizia mafuta katika Kampuni ya Shigongo Oil. Alikuwa mtu mwema sana,
asiyetaka njia za uchochoro. Kila hatua ilikuwa ya haki na uwazi,”
aliema Mwanambuu.
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert Kiondo alikiri kutokea kwa tukio
hilio akisema ameshaingiza ‘vijana’ wake kuchunguza ukweli wa tukio hilo
la kujinyonga au kunyongwa.
Mwili wa
marehemu Gashaza uliagwa juzi nyumbani kwake, Yombo-Vituka, Dar na
kusafirishwa Ngara, Kagera kwa mazishi. Mungu ailaze pema peponi roho ya
marehemu. Amina.Chanzo GPL
Post a Comment