PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SERIKALI YAJIPANGA KUPAMBANA NA MAGONJWA AMBUKIZI NCHINI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Hayo yamesema na Meneja Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bi Anjela Mziray wakati wa mkuatano na waan...




Hayo yamesema na Meneja Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bi Anjela Mziray wakati wa mkuatano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akieleza Bi Anjela amesema kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya imekuwa ikichukua juhudi za maksudi katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na Saratani za aina mbalimbali.

Akifafanua zaidi Bi Anjela amesema programu hiyo imekuja kutokana na ukweli kwamba magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka na yamekuwa tishio na kusababisha vifo vya watu wengi nchini na duniani ambapo takwimu za shirika la afya Duniani za mwaka 2012/2013 watu zaidi ya milioni 35 hufa kwa sababu ya magonjwa yasiyoambukiza.
Bi Anjela aliongeza kuwa kati ya waathirika wa magonjwa yasiyoambukiza milioni 28.1 wanatoka katika nchi zinazoendelea ambapo kwa Tanzania magonjwa hayo husababisha vifo mara 4 zaidi mijini ambavyo ni sawa na asilimia 12.8 wakati asilimia 3.1 wapo vijijini. Akitolea Mfano Bi Anjela alisema katika zoezi la upimaji lililofanyika Dodoma Septemba, 2013 jumla ya watu 591 walipimwa kati yao 14 sawa na asilimia 2.3 waligundulika kuwa na kisukari, na 28 sawa na asilimia 5 walikuwa na shinikizo la damu, wakati watu 128 sawa na asilimia 22 walikuwa na uzito uliokithiri.Bi Anjela aliongeza kuwa katika zoezi lililofanyika Mlimani City Jijini Dar es salaam ocktoba, 2013 watu 450 walipimwa, nusu yao waligundulika kuwa na uzito uliokithiri na katika zoezi lililofanyika Zanzibar watu 273 walipimwa ambapo kati yao watu 10 sawa na asilimia 3.6 waligundulika kuwa na kisukari, watu 83 sawa na asilimia 30.4 walikuwa na uzito uliokithiri.Naye Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja alitoa wito kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora ili kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kama kisukari, msongo wa mawazo na shinikizo la damu.Katika jitihada za Kutoa huduma bora kwa wananchi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebuni mkakati maalum ambao unajulikana kama Afya Bonanza ambayo ni Kampeni ya kupima afya na kutoa elimu juu ya magonjwa yasiyoambukiza na inakusudiwa kufanyika mikoa yote hapa nchini ambapo Zoezi hilo lilizunduliwa rasmi Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam mwezi machi 2014.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top