WIKI mbili kabla ya Tanzania kuadhimisha
miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Makamu Mwenyekiti
mstaafu wa CCM, Pius Msekwa ametoboa siri ya Muungano huo akisema
“mchakato wa kuundwa kwake ulifanywa kwa siri na haraka sana,” kutokana
na upepo wa kisiasa na usalama wa kipindi hicho.
Akizungumza katika
moja ya mfululizo wa vipindi vya miaka 50 ya Muungano vinavyorushwa na
Redio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa), Msekwa alisema woga
wa hayati Abeid Amani Karume kupinduliwa na maadui, ulikuwa ni miongoni
mwa sababu za kuharakisha Muungano huo.
Msekwa aliyekuwa
Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati Muungano unaasisiwa, alisema pia
yeye na wenzake walichelewa kujua kwamba Mwalimu Julius Nyerere (Rais wa
Kwanza wa Tanganyika) na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Karume walikuwa na
majadiliano ya kuunganisha nchi hizo.
“Kikubwa cha kusema
ni kwamba mazungumzo ya Muungano huo yalifanywa kwa siri.... kwa siri
sana baina ya waasisi wa nchi hizo. Kwa nini yalifanywa kwa siri? Siyo
kwa sababu walikuwa wababe, la hasha, bali kwa mazingira ya wakati ule,
kulikuwa na maadui ambao wasingependa nchi hizi kuungana,” alisema
Msekwa na kuongeza:
“Kwa woga huohuo, ndipo Mwalimu
alipokubaliana na mwenzake wafanye mazungumzo ya siri mpaka waliposaini
yale makubaliano na kunijulisha.”
Msekwa ambaye pia amewahi
kuwa Spika wa Bunge la Muungano, alisema baada ya makubaliano ya
Muungano, Nyerere alimwita na kumjulisha kuwa walishakubaliana (na
Karume) kuungana, hivyo walihitaji baraka za Bunge kuridhia Muungano
huo.
“Mwalimu akaniambia, ‘wewe Katibu wa Bunge unaweza ukawaita wabunge wakaja kwa harakaharaka kuridhia makubaliano?’
“Nakumbuka
siku hiyo ilikuwa Jumanne na Mwalimu alipendekeza wabunge wafike Ijumaa
ya juma hilohilo, nao wabunge wakaja wakaridhia.”
Simulizi
hii ya Msekwa kuhusu Muungano imekuja wakati kukiwa na vuguvugu la
muundo wa Muungano katika Bunge Maalumu la Katiba, kutokana na
mapendekezo yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba kupendekeza serikali tatu
badala ya Serikali mbili za sasa.
Bunge kuridhia
Aliongeza
kuwa, baada ya Bunge la Tanganyika kuridhia Mwalimu Nyerere aliutaka
muswada huo “kwa haraka sana” ili aufanye kuwa sheria na alitaka
kupelekewa kwa mkono.
“Baada ya wabunge kuridhia pale Karimjee, nikauchukua muswada na kuupeleka Ikulu, sio mbali pale.
chanzo: MWANANCHI
MZEE MSEKWA AANIKA SIRI YA MUUNGANO
Title: MZEE MSEKWA AANIKA SIRI YA MUUNGANO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
WIKI mbili kabla ya Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Mse...
Post a Comment