Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat), Dk. Didas Masaburi
Kadhalika, Alat imesikitishwa na vurugu na mivutano inayoendelea katika Bunge la Katiba na kueleza kuwa yamerudisha nyuma morali ya wao kwenda bungeni kudai haki zao.
Dk. Masaburu alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam baada ya kutoa taarifa ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa 30 wa ALAT mjini Tanga utakaoanza Mei 7 hadi 10, mwaka huu. Alisema katika mkutano huo wenye kauli mbiu “miaka 30 ya Serikali za Mitaa na ALAT: Katiba bila sura ya serikali za mitaa ni kudhoofisha demokrasia ya wananchi”, utahudhuriwa na washiriki zaidi ya 500.Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo atakuwa Rais Jakaya Kikwete, pia utahudhuriwa na wenyeviti na mameya 168 wa halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya, wakurugenzi, wabunge 25 mmoja toka kila mkoa, wizara, idara za serikali kuu, wakala wa serikali, taasisi, pamoja na mabarozi wa nchi hapa nchini.“Tukienda Dodoma tutawatumia wabunge 25 waliokuwapo katika mkutano waende kutusaidia katika kulipigania suala hilo,” alisema Dk. Masaburi.Alisema mkutano huo ni wa aina ya pekee kwa sababu ALAT inafikisha miaka 30 tangu kuundwa kwake, pia ni miaka 30 tangu Tanzania irudishe tena mfumo wa serikali za mitaa, kadhalika ni mwaka ambao nchi inaunda katiba yake mpya, pia ni miaka 30 tangu aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Moringe Sokoine afariki dunia, na kwamba alitoa mchango mkubwa kwa ALAT.“Hata kama Bunge la Katiba litakuwa limeisha mwezi wa tano, sisi tutaendelea kusema kuwa Serikali za Mitaa zimedhalilishwa kwa kutokuweka katika Katiba mpya, na Tanzania itakuwa nchi ya kwanza duniani kutojali Serikali za Mitaa ,” alisema.
Post a Comment