Wanaotumia bidhaa zitokanazo na Meno ya Tembo matatani! A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: Wanaotumia bidhaa zitokanazo na Meno ya Tembo matatani! Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: KUFUATIA hatari ya kutoweka kwa Tembo katika Mbuga za Wanyama hapa Nchini, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ime... KUFUATIA hatari ya kutoweka kwa Tembo katika Mbuga za Wanyama hapa Nchini, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepiga marufuku bidhaa zinazotengenezwa kwa Pembe za Ndovu, ikiwa ni sehemu ya mpango Mkakati wa kudhibiti Biashara haramu ya Meno ya Tembo Nchini. Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, hivi karibuni alikaririwa akisema kuwa Wizara hiyo imepanga kushirikina kisera na Nchi zinazodaiwa kuwa wadau wakubwa wa Meno ya Tembo ili kuwabani wanaofanya biashara hiyo haramu na kuwachukulia hatua za Kisheria. Kufuatia tamko hilo, Mijadala mbalimbali imekuwepo katoka Mitandao ya Kijamii ikiwemo Jamiiforum na Facebook (pages), ambapo baadhi ya Wananchi wamesema Wizara yenye dhamana inatakiwa ishirikiane na Wakuu wa Kaya, ambao mara nyingi wanafahamu tabia za Wananchi walionao ili kukomesha tabia hiyo. Walisema kuna baadhi ya vinara wanaoshiriki kuua Tembo hao hivyo ihakikishe inamkamata Kiongozi wake aliyeko Mkoani Arusha hivyo, Serikali imfuatilie jangili huyo ilikukomesha suala la uhalifu wa Tembo hapa Nchini. “Serikali iwape Uhuru Wananchi kuwataja Majangili tunaowajua kama Wabunge wanavyowataja wahalifu kwani tunavielelezo, hata Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuna kipindi waliwataja Majangili lakini hawakushughulikiwa” Meno ya Tembo hutengenezea nini? Biashara harama ya Meno ya Tembo kwa hivi sasa imeshika kasi katika maeneo mbalimbali hapa Nchini na nje ya Nchi, ambapo pamoja na Sekta ya Utalii kuanzisha harakati za kuwakamata watu wanaojihusisha na uuzaji wa vitu mbalimbali kwa kutumia bidhaa hizo bado hali inaripotiwa kuwa mbaya katika Mbuga za wanyama. Utafiti unaonyesha meno ya Tembo wanaouwawa katika maeneo mbalimbali hapa Nchini, hutengenezea vitu vya urembo Kama Pete, Bangili, Mikufu na vitu hivyo huvaliwa na watu wakubwa kama wafalme na malkia. Aidha Meno hayo pia hutengenezea Vijiti vya kulia Chakula ambavyo hutumika kwa Nchi za za nje, ambavyo huvitumia pia hutengenezea vinyago (sanamu au picha) mbalimbali za watu maarufu na huuzwa kwa gharama kubwa na kulikosesha Taifa mapato Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori Tanzania (Tawiri), katika utafiti wake inaonyesha kuwa Tembo 30 wanauawa kila siku katika Mbuga mbalimbali hapa Nchini ambapo Taasisi hiyo imesema kuwa miaka ya 60, Tanzania ilikuwa na Tembo kati ya 250,000 hadi 300,000, lakini mpaka kufikia mwaka 2011, kuna tembo 70,000. Kama hali hii itaachwa iendelee kuwa hivyo, Taifa litakuwa limepoteza chanzo kikubwa cha fedha za kigeni zitokanazo na Utalii, na Vizazi vijavyo havitaweza kumuona Mnyama huyo mkubwa Duniani. Watumishi na Vyombo vya dola Hivi karibuni, kuna baadhi ya watumishi katika Vyombo vya dola wakiwamo Askari Polisi na Wanajeshi, ambao wamekuwa wakikamatwa na Meno ya Tembo matukio ambayo yanaelezwa kuwa ni hatari kwa kuwa wao ndiyo walinzi wa usalama na Maliasili za Taifa na kuishia kufukuzwa kazi pasipo Sheria ya Mamlaka husika kuchukua hatua za ziada. Wananchi wanasema nini kuhusu biadhara hii? Wamesema wanajiuliza mara kwa mara kuwa Biashara ya Pembe za Ndovu inawezeshwa na kundi gani, kwani maneno ambayo wamekuwa wakiyasikia kutoka Serikalini hawaoni kama mbinu zinazotumika zitamaliza tatizo hilo kama Serikali haitadhamiria kikamilifu katika kutatua tatizo hilo kwa ktumia Sheria iliyopo. Walesema Usafirishaji wa Pembe hizo na Nyaraka nyingine zinakosesha Serikali Kuu mapato kutokana vyombo vya Kiserikali Vikiwemo Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), havijaonesha nia kwani wahusika hawahukumiwi kutokana na makosa wanayokutwa nayo. Tanzania inafahamika na kuheshimika kutokana na kuwa na raslimali kubwa ya Wanyama pori barani Afrika na Duniani, ambapo sifa hiyo hujumuisha uwepo wa Hifadhi za Tifa 16, Wanyamapori Tengefu 44, Mapori ya akiba 28, maeneo ya Jumuia ya Hifadhi za Wanyamapori (WWs) 38 na Hifadhi za Misitu. Sekta ya Utalii pia imeiingizia Tanzania fedha nyingi za kigeni, kiwango kinachofikia asilimia 17 ya pato la Taifa (GDP).
Post a Comment