SERIKALI IMETAKIWA KUJENGA KLINIK YA WATHIRIKA WA MADAWA YA KULEVYA A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: SERIKALI IMETAKIWA KUJENGA KLINIK YA WATHIRIKA WA MADAWA YA KULEVYA Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: SERIKALI imeshauriwa kujenga Kliniki Maalum kwa ajili ya Vijana wanaoathirika na Dawa za Kulevya, maarufu kama ‘Mateja’ ili kuwarejes... SERIKALI imeshauriwa kujenga Kliniki Maalum kwa ajili ya Vijana wanaoathirika na Dawa za Kulevya, maarufu kama ‘Mateja’ ili kuwarejesha katika hali ya Kawaida Ushauri huo umetolewa na Katibu wa Taasisi inayowasaidia Vijana waliothiriwa na Madawa ya Kulevya inayojulikana kama Taq Complex ya Jijini Dar es salaam, Enok Maregesi, ambapo amesema endapo ushauri huo utafanyiwa kazi tatizo hilo litakuwa limetatuliwa kwa asilimia kubwa Amesema ili kufikia malengo ya kusaidia Vijana hao, mafanikio yaliyopatikana katika Nchi mbalimbali kwa jambo hilo, ni pamoja na jitihada ambazo zilifanywa na Nchi kujenga Kliniki jizo katika kuwasaidia Vijana ambao wameondokana na tatizo hilo. Maregesi amezitaja baadhi ya Nchi kama Tanzania, Afrika ya Kusini, Ghana na Uingereza kuwa ni Nchi ambazo zinakabiliwa na tatizo la Madawa ya kulevya, ambayo yamekuwa tatizo kubwa kwa Vijana walio wengi na kupoteza nguvu ya Familia zilizo nyingi, kukosa ajira na kukata tamaa. Amesema Wazazi wengi wamekuwa wakishindwa kuwapeleka Vijana wao katika Vituo vya Matibabu walioathiriwa na Madawa ya kulevya, kutokana na gharama kubwa na matozo wanayodaiwa katika Vituo hivyo, hivyo kama Serikali itajenga Kliniki hizo kero hiyo itapungua na kuwasaidia Vijana weng
Post a Comment