Hatua hiyo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya msichana mmoja Mtanzania kuuawa kikatili katika mji wa Guangzhou nchini Uchina.
Waziri Membe amesema huenda baadhi ya wahusika wa bishara hiyo ni Watanzania wanaosafirisha wasichana wa dogo kwa kisingizio cha kuwatafutia ajira. Baadhi ya wanaosafirishwa hujipata pabaya baada ya kuwasili Uchina ambapo hunyang'anywa hati zao za usafiri na kulazimishwa kushiriki ukahaba.
Baadhi ya wakaazi wa Dar es laam wameelezea kusikitishwa na vitendo hivyo na kuitaka serikali ichukue hatua.
Post a Comment