SYRIA INASEMA "Tumesikitishwa na Waarabu kushirikiana na Israel" A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: SYRIA INASEMA "Tumesikitishwa na Waarabu kushirikiana na Israel" Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria amesema kuwa,... Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria amesema kuwa, nchi yake inashangazwa na kusikitishwa mno na ushirikiano wa baadhi ya nchi za Kiarabu na utawala haramu wa Israel. Faisal al-Miqdad amesema kuwa, ushirikiano wa baadhi ya nchi za Kiarabu na utawala ghasibu wa Israel na kufanya njama za kufanikisha malengo ya utawala huo bandia katika Mashariki ya Kati ni jambo la kusikitisha mno. Amesema, tangu mwanzoni mwa mgogoro huo, viongozi wa Syria walikuwa wakifahamu vyema kwamba, nchi za Kiarabu hazina ujasiri wa kufanya njama dhidi ya Damascus peke yao na hilo limethibiti sasa kutokana na kushirikiana na Israel na Marekani dhidi ya Syria. Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria amesema kuwa, viongozi wa Damascus hawana shaka kwamba, wananchi, jeshi na uongozi wa nchi hiyo utawashinda maadui wa taifa hilo. Wakati huo huo, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imekosoa vikali himaya ya Uturuki kwa magaidi wanaoingia nchini humo kwa ajili ya kupambana na serikali ya Rais Bashar al-Assad. Katika barua yake kwa Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, serikali ya Syria imelalamikia uvamizi wa ardhi yake unaofanywa na magaidi wanaoungwa mkono na jeshi la Uturuki.
Post a Comment