PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MTIZAME BIBI WA MIAKA 100 AHITIMU ELIMU YA MSINGI!!!!!!!!!!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Bibi mmoja nchini Mexico amefanikiwa kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 100. Bibi huyo Manuela Hernandez (picha...
Bibi mmoja nchini Mexico amefanikiwa kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 100. Bibi huyo Manuela Hernandez (pichani) ambaye alizaliwa katika jimbo la Oaxaca mnamo mwezi Juni 1913, aliacha shule ya msingi baada ya kusoma kwa mwaka mmoja tu na kurejea kuisaidia familia yake masikini kufanya kazi za nyumbani. Hata hivyo alirejea shule kuendelea na masomo mwezi Oktoba mwaka uliopita akiwa na miaka 99 kufuatia kushauriwa na mmoja wa wajukuu zake. Manuela Hernandez akiwa ameshikiliacheti chake cha kuhitimu elimu ya msingi.Hivi sasa tayari amekabidhiwa diplomayake ya elimu ya msingi katika shereheiliyofanyika katika jimbo Mexico Kusini.Bibi Hernandez amesema sasa ataendeleana masomo ya elimu ya sekondari.Zaidi ya nusu ya wakazi wa jimbo laOaxaca wenye umri wa zaidi ya miaka 15hawajamaliza elimu ya msingi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top