Mahakama ya Misri imeahirisha kesi ya mamia ya wafuasi wa
kiongozi aliyeng'olewa madarakani wa nchi hiyo Muhammad Mursi muda mfupi
baada tu ya kuanza katika mji wa Minya.
Zaidi ya wafuasi 500 wa Mursi na wanachama wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ambacho ndicho chama kikubwa zaidi cha siasa nchini Misri, walifunguliwa mashtaka jana kwa tuhuma zinazohusiana na machafuko yanayoikumba Misri tangu mwezi Agosti mwaka jana.
Kesi hii inayowakabili wafuasi 1200 wa Ikhwanul Muslimin ndiyo kubwa zaidi tangu jeshi la Misri lilipomuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muhammad Mursi tarehe 3 Julai 2013.
Miongoni mwa wanaotuhumiwa katika kesi hiyo ni kiongozi wa Ikhwanul Muslimin Muhammad Badie anayeshikiliwa na vyombo vya usalama vya Misri.
Kesi hii ni sehemu ya ukandamizaji unaofanywa na serikali inayoungwa mkono na jeshi ya Misri dhidi ya wafuasi wa chama cha Ikhwanul Musilimin.
Wakati huo huo mahakama nyingine ya Misri jana iliwahukumu wanafunzi 16 wa Chuo Kikuu cha al Azhar kifungo cha miaka mitatu jela kwa hatia ya kushiriki katika maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu. Raia hao wa Misri wanataka kurejeshwa madarakani Mursi ambaye alichaguliwa kupitia kura za wananchi.

Post a Comment