DC; Hatimiliki zitumike kulinda Vyanzo Vya Maji! A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: DC; Hatimiliki zitumike kulinda Vyanzo Vya Maji! Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: MKUU wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akipanda mti katika chanzo cha Maji, kilichopo eneo la Loruvani ikiwa ni njia moja wapo ya... MKUU wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akipanda mti katika chanzo cha Maji, kilichopo eneo la Loruvani ikiwa ni njia moja wapo ya kutunza vyanzo vya Maji ili upatikanaji wake uwe endelevu,kabla ya shughuli ya kuweka Jiwe la msingi katika Ujenzi wa Uzio wa kulinda chanzo hicho kisiharibiwe ambayo ni moja ya shughuli zinazofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Arusha (AUWSA) katika maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana Mkoani Arusha. MKUU wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa, akizindua Jiwe la Msingi wa ujenzi wa uzio wa kulinda chanzo hicho ili kisiharibiwe, shughuli zinazofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka (AUWSA) katika Maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyoanza jana kimkoa Mkoani humo. MKUU wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Nyirembe Munasa, ameagiza Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Arusha (AUWSA) kuhakikisha kuwa inayawekea hatimiliki maeneo yote ya Vyanzo vya Maji yaliyopo Wilayani humo, ili kuzuia vitendo vya uvamizi na uharibifu wa Vyanzo hivyo. Amesema kuwa Serikali haitawafumbia macho wale wote watakaobainika kuyavamia na kuharibu maeneo ya vyanzo vya Maji, na ambapo amesisitiza kuwachukuliwa hatua za Kisheria huku akisema tayari wapo baadhi ya Wananchi katika Kata ya Ngarinanyuki wamechukuliwa hatua hizo kwa kosa la kuharibu Vyanzo hivyo. Munasa akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya maji iliyofanyika katika eneo la Loruvani wilayani humo amesema kuwa uharibifu wa mazingira umekua ni janga kubwa linalotishia vyanzo vya Maji, hivyo amewataka Wananchi kuvitunza vyanzo hivyo kwa kuwa maji ni nyezo muhimu katika shughuli za maendeleo ya jamii kwa ujumla. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa (AUWSA), Fabian Maganga, amewataka Wananchi kutunza vyanzo vya Maji hasa wale wanaozungukwa na vyanzo hivyo ili upatikanaji wa Maji uwe endelevu. “Ndugu Wananchi tunawaomba mshirikiane vyema na Mamlaka yetu katika kulinda na kutunza vyanzo vya Maji na Miundombinu yake ili sote tuweze kunufaika na Maji” Alisema Maganga Naye Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Maji katika Mamlaka hiyo, Sifa Swai, alisema kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni baadhi ya maeneo ya vyanzo vya Maji kumilikiwa kijadi hivyo kuifanya Mamlaka kushindwa kudhibiti uvamizi na uharibifu huo. Hata hivyo amefafanuakuwa, uzalishaji wa Maji umekua ukishuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewana ongezeko kubwa la watumiaji wa Maji Jijini Arusha, na kueleza kuwa Mamlakahiyo imefanya juhudi ya kubaini maeneo mengine ya vyanzo vya Maji ili kuchimba visimavya Maji ili kukidhi mahitaji.
Post a Comment